Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali, Said Mwema (kushoto)
pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki, Zeki
Catalakaya (katikati) wakisaini hati ya ushirikiano wa kuchunguza
matukio ya uhalifu kati ya Tanzania na Uturuki. Kulia ni Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akilishuhudia
tukio hilolililofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es
Salaam leo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi
akiwashukuru kwa furaha ujumbe kutoka nchini Uturuki baada ya kukabidhi
gari maalumu ya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini kwa Jeshi la
Polisi. Gari hilo ambalo linavifaa vyote vya kuchunguza matukio ya
uhalifu nchini lilikabidhiwa leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini
Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi
akiliwasha gari maalumu la kuchunguza matukio ya uhalifu mara baada ya
kukabidhiwa ufunguo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
Uturuki, Zeki Catalakaya. Gari hilo ambalo linavifaa vyote vya
kuchunguza matukio ya uhalifu nchini lilikabidhiwa leo Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (watatu
kutoka kulia-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka
nchini Uturuki pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya
kusaini hati ya ushirikiano wa uchunguzi wa matukio ya uhalifu kati ya
nchi ya Tanzania na Uturuki. Jeshi la Polisi Uturuki tayari limekabidhi
ya gari maalumu la kuchunguza hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Chapisha Maoni