Searching...
Jumamosi, 3 Agosti 2013

RAIS KIKWETE ATOA LA MOYONI KUHUSU RWANDA

RAIS WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU DK.JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Hatimaye Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete ameamua kuvunja ukimya kuhusu vitisho,matusi na kejeli anazozipata kutoka kwa Rais wa Rwanda kuhusu kauli yake aliyoitoa kuhusu kuishauri Rwanda kukaa meza moja na waasi wa nchi hiyo ili kumaliza tofauti zao mezani kuliko kutumia silaha.
akihutubia taifa usiku wa kuamkia leo Rais Kikwete amewahakikishia Warwanda na Watanzania kwamba serikali yake haina nia wala sababu yoyote ya kuharibu uhusiano wa nchi hizi mbili na nchi zote jirani na Tanzania.
"napenda kusisitiza kwamba mimi na serikali yangu ya Tanzania tutakuwa wa mwisho kufanya vitendo vibaya dhidi ya Rwanda au nchi yoyote jirani au nchi yoyote duniani"aliongea kwa hisia kubwa Rais Kikwete.
...."kwa upande wangu binafsi sijasema lolote kuhusu Rwanda,pamoja na maneno mengi kuhusu Rwanda na viongozi wake,pamoja na maneno mengi ya matusi na kejeli yanayotoka kwenye vinywa vya viongozi wa Rwanda sio kwamba sisikii,wala sio kwamba siambiwi yanayosemwa au sio kwamba sijui kusema..la hasha ni kwamba tu sioni faida yake...aliendelea kusisitiza JK.
Rais Kikwete aliendelea kusisitiza kwamba hakuna sababu yoyote ya kukuza ugomvi au mgogoro usiokuwepo.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!