WAYNE ROONEY.
Mshambuliaji wa kimataifa wa England na klabu ya Manchester United Wayne Rooney katika harakati za kutaka kutimka kunako Old Trafford maarufu kama OT amemuambia kocha wake David Moyes kwamba anataka kuondoka klabuni hapo kwani anataka changamoto mpya.na katika kusisitiza hilo amesema ataandika barua rasmi ya kutaka kuondoka mapema wiki hii.
David Moyes anayo matumaini kwamba Rooney ataendelea kusalia klabuni hapo Old Trafford lakini habari za kuaminika kutoka chanzo cha habari hii nikwamba Rooney alimuambia Moyes uso kwa uso kwamba anataka kuondoka mapema tangu walipomaliza ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya huko mashariki ya mbali wiki iliyopita.
JOSE MOURINHO
Lakini pamoja na Rooney kukomalia kwamba anataka kuondoka Manchester United wao wameendelea kushikilia msimamo wao kwamba mchezaji huyo hauzwi kwa klabu yoyote iliyoko ligi kuu England ambapo wanaamini jeuri yote ya Rooney ni kwasababu ya kutaka kutua Chelsea ambapo ameshasema hadharani kuwa anaamini siku moja atafanya kazi na kocha mreno wa Chelsea Jose Mourinho.
SIR ALEX FERGUSON.
Rooney anajua Ferguson alilazimishia suala hilo baada ya kuvunja uaminifu kati ya wawili hao baada ya Ferguson kutangaza kwamba Rooney Mwezi wa nne mwaka jana alimuambia anataka kuondoka Manchester ambapo kwa sasa hata kama Man u watakanusha taarif Now even if United belatedly make a public acknoa hiyo kwamba Rooney hakusema hivyo haitabadili nia yake ya kuondoka.
DAVID MOYES
Lakini wakati Moyes akipasuka kichwa kuhusu Rooney sasa anayo matumaini ya kumnasa kiungo Cesc Fabregas baada ya kiungo huyo kuambiwa na kocha wake mpya Gerardo
Martino kwamba uamuzi wa yeye kurejea ligi kuu England ni uamuzi wa mchezaji yeye mwenyewe.
Martino alisema "ningependa sana kuendelea kuwa naye na aliniambia hataondoka,lakini uamuzi wa ama kubaki au kuondoka ni uamuzi wake yeye mwenyewe... "lakini kama ingekuwa ni uamuzi wangu basi basi ningesema Cesc haondoki"alimalizia Martino.
Martino alisema "ningependa sana kuendelea kuwa naye na aliniambia hataondoka,lakini uamuzi wa ama kubaki au kuondoka ni uamuzi wake yeye mwenyewe... "lakini kama ingekuwa ni uamuzi wangu basi basi ningesema Cesc haondoki"alimalizia Martino.
0 comments:
Chapisha Maoni