Klabu ya Chelsea inaandaa ofa nyingine ya paundi milioni 40 kwaajili ya kumng'oa mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England Wayne Rooney ambapo anatajwa kuwa kama atatua Stamford Bridge basi atakua mshambuliaji chaguo la kwanza la kocha mreno Jose
Mourinho.
Tayari Man u wameshakataa ofa za awali za Chelsea ikiwemo ya paundi milioni 30 lakini Mourinho ameendelea kusisitiza kwamba Rooney ndio chaguo lake la kwanza katika kipindi hiki cha uhamisho na anatarajiwa kuituma ofa hii mpya muda wowote kutoka sasa.
Rooney
ataonekana hadharani kwa mara ya kwanza akiwa na kikosi chaManchester United tangu tarehe 5.5.2013 ambapo anatarajiwa kushuka dimbani wiki ijayo jumanne katika mechi ya kirafiki dhidi ya AIK Stockholm.
Jose Mourinho yupo tayari kufanya lolote ili kumpata Rooney na kumfanya mshambuliaji wake chaguo lake la kwanza kunako Chelse.
Kwa upande wake kocha wa Manchester United David Moyes ameendelea na msimamo wake kwamba Rooney hauzwi japo tayari ameshaweka wazi kwamba hatarajii kumtumia katika kikosi chake cha kwanza na atakaa benchi hadi Robin Van Persie atakapoumia ambapo Rooney amepinga kwamba kiwango chake sio kukaa benchi na anataka kuhakikishiwa kucheza katika kikosi cha kwanza ambapo kama vile kukitia ndimu kidonda tayari Mourinho
amemuhakikishia Rooney kucheza katika kikosi cha kwanza Chelsea na kwa dakika zote 90.
Kocha wa Manchester United David Moyes ameweka wazi kwamba Robin van Persie ndio chaguo lake la kwanza msimu ujao.
0 comments:
Chapisha Maoni