Searching...
Jumatatu, 26 Agosti 2013

MTANDAO WA POLISI WANAWAKE RUVUMA WAWAFARIJI WAGONJWA HOSIPTALI YA MKOA

  Polisi wakike akionyesha mapenzi kwa mtoto aliyoko Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wakati walipotembelea hospitali hiyo na kuwafariji wagonjwa
Askari wakipewa maelezo na Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma  Walta Soko
Askari wa kike akitoa msaada wa kitenge kwa mgonjwa aliyelala kitandani hapo

Na Nathan Mtega wa Demashonews,Songea

MTANDAO  wa polisi wanawake mkoani Ruvuma umeanza maadhimisho ya wiki ya polisi wanawake kwa kutembelea na kutoa msaada kwa wagonjwa wanawake na watoto katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea.
Akizungumza mwenyekiti wa mtandao huo wa polisi wanawake Mrakibu msaidizi wa polisi Anna Tembo amesema lengo la kutembelea katika hospitali hiyo ni kutoa msaada kidogo pole na hongera  kwa wagonjwa waliolazwa ambao ni wanawake waliojifungua  watoto chini ya umri wa miaka mitano pamoja na kuwafariji wagonjwa kwa ujumla.
Amesema pia ni kuifanya jamii itambue kuwa polisi ni sehemu ya jamii ambayo inapaswa kushirikiana na jamii kwa kila jambo na si kwa masuala ya kulinzi na usalama wa watu na mali zao pekee na ushirikiano huo unapaswa kuwepo kwenye idara zote na jamii kwa ujumla.
Amesema kuwa kumekuwepo na matukio mengi ya ukatili kwa watoto yanayofanywa na wazazi ambao ni wanawake na wanaume hivyo maadhimisho hayo yatatumika pia kwa kuifanya jamii kujenga upendo miongonimwao na hasa kwa watoto ambao wamekuwa ndiyo waathirika wakubwa wa matukio hayo ukatili ambao umekuwa ukifanywa na wazazi wao kwa sababu mbali mbali huku baadhi ya wanawake wakiwatupa watoto wao baada ya kujifungua kwa kushirikiana na wanaume baada ya kudanganyana kuhusu kuoana.
Mwenyekiti wa mtandao huo pamoja na kuiasa jamii kuhusu vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake ambavyo baadhi vimekuwa vimekuwa vikitokea kwa sababu ya kukosekana kwa upendo kwa wanandoa ameshauri kuutumia mtandao huo wa polisi ambao unafanya kazi kwa ushirikiano na kituo cha msaada wa kisheria cha mjini Songea kwa kuwsilisha matatizo yao mbali mbali ili yaweze kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya amani.
Akizungumzia ujio huo wa askari polisi wanawake hospitalini hapo Afisa muuguzi kiongozi wa hospitali hiyo  Marcella Wella mbali ya kuwashukuru askari polisi hao kwa uamuzi huo lakini ameiomba jamii kutambua kuwa polisi nao ni sehemu ya jamii na wanaonesha ushirikiano mkubwa na jamii inapaswa kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
Amesema kuwa jamii imekuwa na mtazamo hasi kwa askari wa jeshi la polisi kwa kujengeka na imani kuwa askari polisi wapo kwa ajili ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao tu lakini kitendo cha askari polisi hao kupitia mtandao wao kufika na kuwafariji wagonjwa wakiwemo wanawake na watoto kwa kutoa msaada wa vitu mbali mbali zikiwemo sabuni,madishi na nguo ni ishara kuwa askari polisi nao ni wana jamii ambao wnaonesha ushirikiano mkubwa na jamii wanayoitumikia hivyo ni wajibu wa kila mmoja kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
Naye mkuu wa kituo kikuu cha polisi cha mjini Songea mrakibu msaidizi wa polisi  Mashimbi ameitaka jamii kukitumia kitengo hicho cha mtandao wa polisi wanawake kwa kutoa malalamiko yao yanayohusiana na unyanyasaji wa aina yoyote kwa sababu vitendo hivyo vipo kwa kila mmoja na si kwa wanawake pekee.
Amesema kuwa zipo taarifa za wanaume kunyanyaswa na wanawake lakini wamekuwa wakiona aibu kutoa taarifa za unyanyasaji wanaofanyiwa hali ambayo hupelekea kujichukulia sheria mkononi na kuleta madhara makubwa kwa wanafamilia hivyo ni vyema wakautumia mtandao huo wa polisi wanawake kutatua matatizo yao na kujenga utamaduni wa upendo miongoni mwao.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!