Searching...
Alhamisi, 8 Agosti 2013

KAMA ULIKOSA KUZIONA PICHA ZA TAJIRI WA ARUSHA ALIYEUWAWA KWA KUPIGWA RISASI JANA HIZI HAPA NA HABARI ZAKE ZA AWALI

 Hilo ni gari la Marehemu ambalo alikua akisafiria kutoka arusha kwenda Moshi,na alipofika maeneo hayo ya njia panda ya Uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA akapaki hapo unapoliona gari na kisha kushuka na kuongea na watu ambaoa alikua na miadi nao na kisha katika hali isiyo ya kawaida baada ya kushindwa kuelewana wakamshambulia kwa bunduki aina ya SMG kwa zaidi ya Risasi 10.
 Mwili wa marehemu baada ya kushambuliwa na watu wanaodhaniwa ni majambazi ukionyesha matundu ya risasi mwilini.
Watu wa usalama wa taifa wakiukagua mwili wa marehemu Erasto Msuya baada ya kumiminiwa risasi nyingi mwilini na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi japo habari za kuaminika hawakuiba kitu chochote zaidi ya kumuua na kuondoka na piki piki.
 
Hapa mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari la polisi tayari kupelekwa Mochwari chini ya ulinzi mkali wa polisi

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!