Msanii
Muigizaji wa filamu na muziki wa bongo fleva, Shilole pichani kushoto
akiimba mbele ya maelfu ya wakazi wa Singida waliojitokeza kwa wingi
kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2013, ndani ya Singida Motel.
Sehemu ya umati wa watu wakishangilia burudani iliyokuwa ikiendelea kwenye kiota hicho cha Singida Motel.
Mkongwe
wa muziki wa kizazi kipya, Sir Juma Nature akiwa na wasanii wenzake wa
kundi la TMK -Wanaume Halisi, wakilishambulia jukwaa vilivyo.
Anajiita
Raisi wa Manzese, kutoka kundi la Tip Top Connections, Madee
akiwaimbisha mashabiki wake, ndani ya Singida Motel wakati Tamasha la
Serengeti Fiesta 2013 likiendelea.
Mashabiki
waliokuwa wamejibanza ubavuni mwa jukwaa,nao walikuwa wakipata ile kitu
roho inapenda kutoka kwa wasanii mbalimbali waliokuwa wakitumbuiza
jukwaani.
Pichani
kulia ni Niki wa Pili na shoto ni kaka yake Joe Makini, wote ni wasanii
wa muziki wa kizazi kipya a.k.a hip hop wakiwa sambamba na mtangazaji
wa Clouds FM, Adam Mchomvu wakishangilia jambo nyumba ya jukwaa.
Chumaaaa a.k.a Chid Benz akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani.
Sehemu ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya Singida Motel, mkoani Singida.
Anajiita
mzee wa Mahaba kutoka Manzabay, Cassim Mganga akiimba nyimbo zake za
mahaba, mbele ya maelfu ya wakazi wa singida na vitongoji vyake
waliojitokeza kwenye tamasha hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
Ommy Dimpo a.k.a pozi kwa pozi akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani.
Kutoka kundi la Wanaume TMK, Chege na Themba wakilishambulia jukwaa.
Dj
Mahiri kutoka Clouds FM, Dj Zero akifinya finya mashine zake kwa namna
ya pekee kabisa, iliyokuwa ikiwafanya mashabiki kibao wazidi kuchenguka
na kupiga mayowe kila wakati.
Wenywewe
wanajiita Makomando, wakilishambulia jukwaani kwa pamoja usiku huu
wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea ndani ya Singida
Motel.
Ni full kujiachia usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013, wengine wakiwa juu ya miti aaahhh nomaa sanaaa.!
Baadhi
ya wakazi wa mkoa wa Singida wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu
kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 linalofanyika kwenye viwanja vya
Singida Motel usiku huu.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Peter Msechu akiwaimbisha mashabiki wake
waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta
2013 linaloendelea hivi sasa ndani ya Singida Motel.
Ni ndani ya Singida Motel tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea hivi sasa
Wasanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT, Lina na Amin
wakilishambulia jukwaa kwa pamoja, huku wakazi wa Singida waaliofurika
usiku huu ndani ya Singida Motel wakipiga mayowe ya shangwe.
Amin
Jukwaani akiwambisha mashabiki wake, huku mayowe kila kona yakisikika
usiku huu ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya Singida
Motel, mkoani Singida.
Ni burudani Serengeti Fiesta nomaa sanaaa usiku huu.
0 comments:
Chapisha Maoni