Searching...
Alhamisi, 1 Agosti 2013

USAJILI ULAYA-SOLDADO ATUA TOTTENHAM KWA PAUNDI MILIONI 26.

Roberto Soldado 
ROBERTO SOLDADO.
Klabu ya Tottenham Hotspur imekubali kuvunja rekodi ya usajili wake baada ya kukubali kutoa kiasi cha paundi milioni 26 ili kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Valencia Roberto Soldado.
Taarifa kutoka klabuni hapo zinasema mchezaji huyo atasaini mkataba mrefu wa miaka minne na kuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa Tottenham msimu huu ambapo anatarajiwa kukamilisha vipimo vya afya kesho ijumaa 
Soldado mwenye umri wa miaka 28, aliwahi kuchukua vikombe 11 akiwa na timu ya taifa ya Hispania na kufunga magoli 30 baada ya kushuka dimbani mara 46 ligi kuu ya Hispania La Liga akiwa na klabu yake ya valencia  msimu uliopita.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!