Watu wanne wamefariki dunia na wawili kati yao kujeruhiwa vibaya leo asubuhi jijini Dar es salaam baada ya magari yao waliyokuwa wakisafiria aina ya Suzuki Carry yenye nambari za usajili T 180 BWY na toyota land cruser lenye nambari za usajili STK 4433 kugongana uso kwa uso maeneo ya boko nje kidogo ya jiji la dar es salaam.
Akizungumza na MCHOME BLOG kamanda wa polisi mkoa
wa kipolisi wa kinondoni kamanda CAMILIUS
WAMBURA amesema ajali hiyo imetokea wakati wa asubuhi majira ya sa kumi na moja ambapo gari aina ya land cruiser lilikua likitokea Tegeta kwenda Boko na gari dogo likitokea boko kwenda mjini ambapo inadaiwa mmoja kati ya madereva alitaka ku-overtake gari lingine kisha wakakutana uso kwa uso.
Ameongeza kuwa dereva wa gari dogo amefariki dunia na mwingine wa land cruiser anaendelea vizuri kidogo ila amesema majeruhi mwingine ana hali mbaya na amelazwa katika hosiptali ya mwananyamala.
kuhusu utambuzi wa miili ya marehemu ambayo ipo mwananyamala hosiptali bado haijatambuliwa na hivyo kutoa rai kwa watu kujitokeza kuitambua miili hiyo
jitihada za kupata picha za eneo la ajali zinaendelea na utazipata punde hapa hapa MCHOME BLOG
0 comments:
Chapisha Maoni