Kutoka kushoto ni Tatu Issa mwanafunzi wa chuo kikuu cha SAUTI tawi la Songea , Tamimu Adam mtangazaji wa Radio Jogoo FM na Aneth Mponda mwanafunzi wa chuo kikuu cha SAUTI tawi la songea wakiwa wanajadili mada inayohusu matumizi ya mitaandao ya kijamii katika kipindi cha Jamvi letu kinachoendesha na kituo hicho cha radio katika manispaa ya songea Mkoani Ruvuma'
  Aneth akielezea faida anayoipata kupitia mitandao ya kijamii hasa Facebook ambayo kwake ni rahisi kutumia ikiwa ni kubadilishana mawazo ila kwa upande wa Twitter kwake inamuwia ngumu kuitumia kutokana na ilivyo , kwa upande wa changamoto anazokutana nazo amesema " kuna watu humu katika mitandao hutumia sivyo mara kwa mara unakuta wanakutaka kimapenzi na ukimkatalia bado hakomi kila akikuona upo hewani lazima akutumie ujumbe wa mapenzi wakati umemkatalia yeye anakung'ang'nia pia kuna baadhi huweka picha za ngono amabazo ni kinyume na maadili ya kiTanzania unakuta ni mtu mzima na haendani na matendo anayoyafanya pia kuana wengine hawajiamini  wanaweka picha si zao " alisema.
 Tamimu Adam akisikiliza kwa makini mawazo toka kwa washiriki wa kipindi cha Jamvi letu
Tatu Issa akielezea faida ya matumizi ya mitandao ya kijamii  kwa upande wake ni kupata taarifa mbalimbali pia kubadilishana mawazo na marafiki mbali mabali na kupata marafiki kupitia mitaandao pia kwa siku anasema anaingia mara mbili na hutumia zaidi ya  masaa matatu na moja ya mtandao anaopenda ni facebook .
" Japo natumia mitandao hii ya kijamii lakini bado siiyamini kwani kuna baadhi huweka habari zisizo za ukweli mfano kuhusu mitandao ya kijamii iliyozusha juu ya kifo cha msanii Saida kaloli " alisema