LUIS SUAREZ.
Liverpool wamekataa ffa ya klabu ya Arsenal ya paundi milioni 30 kwaajili ya kumnunua mshambuliaji wao nguli Luis Suarez.
Suarez amekuwa katika hali ya kutokuwa na raha na klabu ya Liverpool baada ya kufungiwa kucheza mechi kumi baada ya kumng'ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic katika uwanja wa Anfield msimu uliopita.
Real Madrid waliweka wazi matarajio yao ya kumchukua mshambuliaji huyo wa Uruguai mwenye umri wa miaka 26 baada ya Suarez kuweka wazi kwamba hana raha na maisha ya England
Chelsea nao pia walionyesha nia ya kumsajili Suarez baada ya kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuendeleza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Madrid Gonzalo Higuan
DAVID VILLA.
Mshambuliaji wa Barcelona David Villa tayari ameshaafikiana na klabu ya Tottenham kuhamia klabu hiyo kukipiga msimu ujao na sasa kilichobaki ni vilabu hivyo viwili kukubaliana ada ya uhamisho wake
klabu ya Tottenham wametoa ofa kwa klabu ya Barcelona japo haikufikia kiasi kinachotakiwa na mabingwa hao wa Uhispania cha paundi milioni 8.6
Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy anaamini wanaweza wakapunguza kiasi hicho cha pesa kwasababu Barcelona wanataka kumuuza Villa kwasababu hawapo tayari kumlipa Villa mshahara wa paundi milioni 110,000 kwa wiki wakati anaweza akaondoka bure mwezi wa tano mwakani wakati mkataba wake utakapomalizika.
ROBERT LEWANDOWSKI.(kulia)
Kocha wa Dortmund Jurgen Klopp amemaliza uvumi na tetesi za mchezaji wake Robert Lewandowski baada ya kuthibitisha kwamba mchezaji huyo atahamia kwenye klabu ya Bayern Munich mwakani.
Mwanzoni mwa msimu wa uhamisho kuanza mchezaji huyo aliweka wazi matamanio yake ya kujiunga na mabingwa wa ulaya na ujerumani Bayern , japo Dortmund walikataa kwamba mchezaji huyo hauzwi msimu huu na hata kama akiuzwa sio kwa vilabu vya ujerumani.
Manchester
United na Chelsea walionyesha nia ya dhati ya kumsajili mchezaji huyo aliyeonyesha kiwango kikubwa msimu uliopita hasa katia ligi ya mabingwa wa ulaya lakini sasa Klopp amekubali yaishe kwa kukubali kwamba ataendelea kukipiga klabuni hapo msimu ujao alafu ndio ataruhusiwa kutua Allianz Arena mwakani.
0 comments:
Chapisha Maoni