Naibu  Waziri Angellah Jasmine Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi  rasmi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na  Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi   na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za  mikononi. 
 
Mkurugenzi  Mtendaji wa Push Media Mobile, Freddie Manento akifafanua jambo katika  wakati wa uzinduzi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili  Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu  za mkononi  na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia  simu zao za mikononi. kulia ni Naibu Waziri Angellah Jasmine Kairuki na  kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko.
 
NAIBU  Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Angellah Kairuki amezindua huduma  ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA)  ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi  na mtandano  kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi.  
  
Katika  huduma hiyo, wananchi wataweza kupata huduma zote zinazotolwa na RITA  kwa kuchagua kipengele anachotaka baada ya kutuma neno RITA kwenda namba  15584 na kupokea muongozo utakaomwezesha kujua utaratibu wa kusajili  kizazi au kifo kilichotokea hospitali na kwengine.  
  
Pia  wanaweza kupata taraifa zao mbali mali kwa kutembelea tovuti ya wakala  hao,  www.rita.go.tz, kwa kujiunga na mtandao wa kijamii wa www.facebook.com/ritatanzania na www.twitter.com/ritatanzania.  
  
Akizungumza  katika uzinduzi huo, Waziri Kairuki alisema kuwa huduma hiyo itapunguza  msongamano wa wananchi kujua taarifa mbali mbali za vizazi na vifo na  nyinginezo zinaztotolwa na wakala hao.  
  
Waziri  Kairuki alisema kuwa huduma hiyo ni kwa nchi nzima na kuipongeza RITA  kwa kushirikiana na Kampuni ya Push Media Mobile kwa kutengeneza huduma  hiyo yenye ubora wa hali ya juu.  
  
“Huduma  hii ni muhimu sana kwa  wananchi na itasaidia kwa kiasi kikubwa  kupunguza gharama za kusafiri umbali mrefu ili kupata taarifa hizo, sasa  taarifa utazipata kiganjani, tena kwa kutumia simu yako ya mkononi, ni  jambo la faraja na la kujivunia,” alisema Waziri Kairuki.  
  
Alisema  kuwa Wizara yao ina mpango wa kuanzisha utaratibu ambao utaongeza kasi  ya usajili wa wananchi kwa wakala hao ambapo mwananchi hataweza kupata  kazi mpaka awe na cheti cha kuzaliwa. Pia hata kwa watu wanaotaka kupata  leseni za biashara, kujiunga na shule na shughuli nyingine mbali mbali  watalazima kuwa na cheti cha kuzaliwa.  
  
Afisa  Mtendaji Kuu wa RITA, Phillip Saliboko alisema kuwa wameamua kujiunga  digitali ili kwenda na wakati na mpango wao mkubwa ni kupanua wigo wa  huduma zao kwa kaya zote.  
  
“Tunataka  kuwa karibu zaidi na kushirikiana na umma, kwa kutumia tovuti, mitandao  ya kijamii na simu za mkononi kama njia ya kuwasiliana na kusambaza  taarifa muhimu kwa wananchi, hii itaturahisishia hata sisi kujua ufanisi  wa shughuli zetu na kukabiliana na changamoto mbali mbali,” alisema  Saliboko.    
  
Saliboko  alisema kuwa kutokana na ongezeko la watumiaji wa intaneti, mitandao ya  kijamii na simu za mkononi, RITA iko tayari kwenda sambamba na  mabadiliko hayo na kutoa jukwaa la mawasiliano baina yao na wananchi.
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni