JAJI KORTI YA RUFANI KUONGOZA KAMATI TFF
Shirikisho  la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani  Tanzania, Bernard Luanda kuongoza Kamati ya Rufani ya Uchaguzi kufuatia  mabadiliko ya Katiba yaliyofanywa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) na  kuingiza kamati nyingine mpya.
 Rais  wa TFF, Leodegar Tenga ametangaza wajumbe wa kamati hizo leo (Julai 18  mwaka huu) mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF  kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Amesema  uteuzi wa wajumbe hao umezingatia maoni ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa  TFF, lakini vilevile amewashukuru wajumbe walioteuliwa kwa kukubali  kutoa mchango wao katika maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
 bali  ya Jaji Luanda ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, wajumbe ni Francis  Kiwanga (Makamu Mwenyekiti), Anney Semu, Yohane Masalla na Allen  Kasamala. Kamati ya Uchaguzi inaongozwa na Hamidu Mbwezeleni, Moses  Kaluwa (Makamu Mwenyekiti), Mustafa Siyani, Hassan Dyamwale na Kitwana  Manara.
 Mwenyekiti  Kamati ya Rufani ya Maadili ni Jaji Steven Ihema, Bi. Victoria Makani  (Makamu Mwenyekiti), Mheshimiwa Mohamed Missanga, Henry Tandau na  Mheshimiwa Murtaza Mangungu. Kamati ya Maadili inaundwa na Bi. Jesse  Mguto (Mwenyekiti), Francis Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Profesa Mtambo  Madundo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Mohamed Mpinga na Evod Mmanda.
 Profesa  Mgongo Fimbo anaongoza Kamati ya Rufani ya Nidhamu wakati Makamu wake  ni Ong’wanuhama Kibuta na wajumbe ni Kanali Mstaafu Idd Kipingu, Dk.  Mshindo Msolla na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mstaafu  Jamal Rwambow. Kamati ya Nidhamu inaongozwa na Kamishna wa Polisi (CP)  Mstaafu Alfred Tibaigana, Mustafa Kambona (Makamu Mwenyekiti),  Mheshimiwa Azzan Zungu, Yusuf Nzowa na Mohamed Msomali.
Pia  Kamati ya Utendaji imefanya mabadiliko katika Kamati ya Waamuzi ambapo  Said Nassoro na Charles Ndagala kutoka Chama cha Waamuzi wanachukua  nafasi za Joan Minja na Riziki Majala. Kamati hiyo inaendelea kuongozwa  na Kapteni Mstaafu Stanley Lugenge, Omar Kasinde (Makamu Mwenyekiti)  wakati mjumbe mwingine ni Mohamed Nyama.
 Kamati  ya Tiba inaongozwa na Dk. Paul Marealle wakati nafasi ya Makamu  Mwenyekiti itajazwa baadaye na Rais Tenga. Wajumbe ni Mwanandi  Mwankemwa, Anthony Ngome, Frank Mhonda, Kapteni Joakim Mshanga na Helen  Semu.
 Rais  Tenga alisema mabadiliko mengine yamefanyika kutokana na waliokuwa  wajumbe kuomba kupumzika. Wajumbe walioomba kupumzika ni Dk. Sylvester  Faya, Idd Mtiginjola na Deo Lyatto 
 Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni