Kocha mkuu wa Manchester United David Moyes leo hii jumanne ameweka mezani majina ya wachezaji wake nane ambao hawahitaji katika kikosi chake msimu ujao ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kuongeza kipato cha klabu ili kununua wachezaji wengine watakaoisaidia timu msimu ujao
David Moyes yupo tayari kusikiliza ofa kwa wachezaji nane ambao ni Luis Nani,
Anderson, Bebe, Kiko Macheda, Anders Lindegaard ,Fabio, Ryan Tunnicliffe na Scott Wootton.
Tayari vilbu vya Arsenal,Juventus,Roma na Anzi vimeonyesha nia ya kumtaka Luis Nani ambaye anaonekana kuwa na thamani ya paundi milioni 8
Anderson naye ameonekana kutakiwa na timu mbalimbali za Ureno kama vile Benfica na Porto wakati klabu ya Santos ya Brazil nayo imeonyesha nia ya kumnyakua mchezaji huyo.
Mnchester United wanaamini kumuuza kinda wao Bebe wanaweza wakapata kiasi cha paundi milioni 2 wakati wakiwa tayari kumuachia huru mchezaji wao Macheda kama atapata klabu atakayoipenda
Mlinda mlango Lindegaard, ambaye alionekana kuchanganyikiwa msimu uliopita baada ya kusugua bench huku mwenzake David de Gea akianza kila mechi amesema yupo tayari kubaki Man u ila anaweza kuondoka endapo tu atapata timu kubwa itakayomuhakikishia kucheza kikosi cha kwanza.
0 comments:
Chapisha Maoni