Searching...
Jumamosi, 13 Julai 2013

SIWEZI KUZUNGUMZIA UHAMISHO WA SUAREZ-WENGER



ARSENE WENGER.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger leo amekataa kata kata kuzungumzia uhamisho wa mshambuliaji wa Liverpool Suarez.
Arsenal tayari walishatuma ofa ya paundi milioni 30 Liverpool wakaikataa sasa Arsenal wameongeza hadi paundi milioni 35 lakini leo hii akiwa na vijana wake nchini Indonesia kwenye maandalizi ya msimu ujao wa ligi Wenger amekataa kuzungumzia hilo.
“Suarez? kama mnavyojua kipindi cha usajili ni kipindi kinachohitaji usiri mkubwa na kutoongea ovyo..kwahiyo siwezi kulijibu swali hilo”Wenger aliwaambia waandishi wa habari nchini Indonesia hii leo.
Tayari bodi ya wakurugenzi wa Aresenal wamemkabidhi Wenger kiasi cha paundi milioni 70 ili kukiimarisha kikosi chake msimu ujao.
Wenger alilazimika kuhamishia nguvu zake kwa Suarez baada ya mipango ya kumnasa Gonzalo Higuainkutoka Real Madrid kugonga mwamba kutokana na kiwango kikubwa walichohitaji Madrid lakini pia kocha mpya Carlo Ancelotti anamuhitaji muajentina huyo kuitumikia klabu hiyo msimu ujao.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!