Taarifa za kuaminika kutoka nchini Italia zinasema Klabu ya Chelsea imebakisha siku chache sana kumtangaza rasmi mchezaji wa klabu ya Roma Daniele De Rossi kwa mkataba wa muda mrefu.
Mchezaji huyo kiungo mkabaji amekuwa akiwaniwa kwa miaka mingi na vilabu vya England kama vile Manchester United ,na Manchester City lakini inaonekana Chelsea waliongeza juhudi hadi kufikia hatua hii.
kiungo mwingine ambaye tayari ameshafungasha virago vyake Chelsea ni Oriol Romeu ambaye amejiunga na klabu ya Valencia kwa mkopo wa muda mrefu na Obi anaonekana kuwaniwa na klabu ya Monaco ya Italia
Danielle De Rossi ameshuka dimbani mara 306 akiwa na klabu yake ya Roma tangu mwaka 2001
0 comments:
Chapisha Maoni