Generali Abdul Fattah al-Sisi akizungumza moja kwa moja kutoka televisheni ya taifa ya Misri
Hatimaye jeshi la Misri limejitokeza live kwenye televisheni ya Misri na kutangaza rasmi kuifuta katiba ya nchi hiyo muda mfupi kutoka sasa
Generali Abdul Fattah Al-Sisi, amesema kuanzia sasa mwanasheria mkuu wa mahakama ya katiba ndiye atakuwa anakaimu madaraka yote ya raisi na kutangaza rasmi kutomtambua bwana Mohamed Morsi
Wapinzani wa raisi Morsi waliandamana na kukusanyika katika uwanja wa Tahrir Square na kuonekana wakishangilia kwa nguvu wakati Generali Abdul akitoa tangazo hilo la kumpindua raisi Morsi
Mchakato huo wa kumng'oa bwana Morsi ni kufuatia maandamano ya umma ya siku nne kumtaka raisi huyo aachie madaraka na kutii amri ya jeshi ambayo imeisha usiku wa leo jumatano saa nne usiku kwa saa za Tanzania
Aidha kituo cha TV kilichokuwa kikimilikiwa na bwana Morsi cha Muslim Brotherhood kilizimika sekunde chache baada ya Generali Abduli kumaliza hotuba ya kumpindua rais MORSI aliyeingia madarakani baada ya kumpindua aliyekuwa raisi wa nchi hiyo HOSN MUBARAK.
Maelfu ya wamisri wakishangilia kwa furaha huku wakipiga mafataki hewani baada ya mkuu wa majeshi kutangaza rasmi kumpindua rais Morsi

Picha hii inaonyesha enzi hizo mwaka mmoja uliopita wamisri walivyokuwa wakimshangilia bwana Mursi kuwa rais wao ghafla tu mwaka mmoja hawamtaki na jeshi limempindua

Picha hii inaonyesha enzi hizo mwaka mmoja uliopita wamisri walivyokuwa wakimshangilia bwana Mursi kuwa rais wao ghafla tu mwaka mmoja hawamtaki na jeshi limempindua
Hapa wanampongeza mmoja wa mwanajeshi baada ya mkuu wa majeshi kutangaza mapinduzi jana usiku
Rais Morsi aliyepinduliwa
Askari wakiwa tayari kwa lolote
0 comments:
Chapisha Maoni