Klabu ya Chelsea imekualiana na klabu ya Vitesse Arnhem kumnunua mchezaji wao kiungo Marco van Ginkel mwenye umri wa miaka 20,Van Ginkel anakuwa mchezaji wa pili kwa Jose Mourinho kusaini mkataba wa kuichezea Chelseabaada ya kumnyakua mshambuliaji Andre Schurrle.
Wakati huo huo Chelsea wamesema wapo kwenye mchakato wa mwisho wa kumnyakua kiungo wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Roma Daniele De Rossi kama moja ya mikakati ya mreno Jose Mourinho kutaka kuimarisha safu yake ya kiungo,japo kununuliwa kwa muitaliano huyo sasa Mikel Obi anakuwa katika njia panda ya kuondoka klabuni hapo.
Timu ya Real Madrid imeweka wazi kwamba uwezekano wa kumnyakua au kupata saini ya Gareth Bale kwaajili ya msimu ujao ni ngumu kutokana na msimamo wa klabu yake ya Tottenham kwamba Bale hauzwi, Florentino Pérez pamoja na benji lake la ufundi wamesema wamenyoosha mikono kwa Bale.
WAYNE ROONEY.
Hatimaye katika hali ya kukubali yaishe timu ya Manchester United imemuambia Wayne Rooney kwamba kama anataka kuhama klabu hiyo ni lazima aandike barua rasmi ya kiofisi kwamba anataka kuondoka Manchester United.
Mshambuliaji huyo wa Old Trafford ambaye hapo awali ilisemekana kwamba atakuwa na mkutano rasmi na kocha wake David Moyes kuhusu mustakabali wake ndani ya Man U,sasa taarifa zimeenea kwamba hataki mkutano na mtu yoyote zaidi ya kuondoka.
DAVID MOYES.
Hatimaye katika hali ya kukubali yaishe timu ya Manchester United imemuambia Wayne Rooney kwamba kama anataka kuhama klabu hiyo ni lazima aandike barua rasmi ya kiofisi kwamba anataka kuondoka Manchester United.
Mshambuliaji huyo wa Old Trafford ambaye hapo awali ilisemekana kwamba atakuwa na mkutano rasmi na kocha wake David Moyes kuhusu mustakabali wake ndani ya Man U,sasa taarifa zimeenea kwamba hataki mkutano na mtu yoyote zaidi ya kuondoka.
Moyes anasema bado anayo matumaini ya Rooney kuendelea kukipiga OT msimu ujao kwani anachokitaka Rooney ni kubatilisha kauli iliyotolewa na Ferguson kwamba hataki kuendelea kuichezea Man U kauli ambayo Rooney imemuumiza sana na kutaka aombwe radhi vinginevyo anasepa(anaondoka) kauli ambayo kwa jinsi Manchester United wanavyomuheshimu Sir Allex wanaona kumuomba radhi Rooney ni kumdhalilisha Babu.
Wakati Rooney akileta sokomoko la kutaka kuondoka Man U,tegemeo lao lingine la kumrejesha Christian Ronaldo limeota mbawa baada ya Ronaldo mwenyewe kujitokeza hadharani na kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu mustakabali wake
‘kwakweli naikumbuka sana ligi kuu ya England. Kwangu mimi ndiyo ligi ambayo sitaisahau maishani mwangu kwa kipindi chote nilipokuwa pale naichezea Manchester United. Bado ni klabu ambayo ipo moyoni mwangu. kweli naikumbuka sana. Lakini sasa maisha yangu yapo hapa Hispania.nafurahia kucheza hapa pia.huwezi kujua ya mbeleni "alisema Ronaldo
STEVAN JOVETIC
Klabu ya Arsenal na Manchester City wameendelea na vita yao ya kumgombea mchezaji nyota wa klabu ya Fiorentina Stevan Jovetic.
timu hizo mbili za ligi kuu ya England zimeonyesha nia ya kumata mchezaji huyo na kila mmoja hataki kushindwa vita hiyo ambapo tayari klabu yake imeweka wazi na kufungua milango kwa klabu yoyote inayomtaka ipeleke ofa yake ili ijadiliwe
JOHN RUDDY.
Matajiri wa london Chelsea wamesema wapo karibu kumnyakua golikipa wa Norwia mlango wao Peter Cech.
0 comments:
Chapisha Maoni