Hatimaye mshambuliaji nguli wa timu ya taifa ya Ureno na klabu tajiri ya uhispania ya Real Madrid ameweka wazi hii leo kwamba hana mpango wala nia ya kuhamia au kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya England ya Manchester United kwasababu kwa sasa akili yake yote ipo Real Madrid.
"Nina furaha kubwa kuwepo hapa Madrid,kwakuwa hapa ndipo maisha yangu yalipo hivi sasa...hakuna ubishi kwamba ninaipenda sana klabu yangu ya zamani ya Manchester United,na ninaikumbuka daima lakini hakuna jinsi zaidi ya kuiweka akili yangu na mawazo yangu Real Madrid" alinukuliwa CHRISTIAN RONALDO
0 comments:
Chapisha Maoni