Picha na maktaba
Joyce Joliga,Songea
WAUMINI wa kanisa katoriki Matogoro Manispaa ya Songea wameshauriwa kuacha
uchoyo na badala yake kujenga tabia ya kusaidiana wao kwa wao bila
kutegemea misaada toka kwa wafadhili wan je ya nchi kwani vitendo hivyo
vimepitwa na wakati.
Ushauri huo umetolewa jana na Paroko msaidizi wa kanisa katoriki la
Matogoro Nicolas Mlelwa ambaye amesema,waumini hao wanapashwa kuacha mkono wa
birika na wajifunze kusaidiana na kufanya mambo yao wao wenye bila kutegemea
wafadhiri.
Amesema,anasikitishwa kuona waumini wa nyanda za juu kusini si watu wa
kujitoa tofauti na majimbo mengine ambapo wamekuwa wakiwasaidiana wao kwa wao
ikiwa ni pamoja na kuwasaidia mapadri wao
“ Nawaomba waumini muache mkono wa birika, mjenge tabia ya kushirikiana na
muanze kujitegemea kwa kusaidiana nyinyi kwa nyinyi ikiwa ni pamoja na
kuwasaidia mapadri wenu kwani kuendelea kutegemea wafadhili si kitu
kizuri bali tuendelee kujitolea kwa moyo wa upendo ,”alisema
Aidha,amewataka waumini hao kuhakikisha wanachangia harambee ya kongamano
la vijana wakatoriki ambalo linatarajiwa kufanyika mapema mwezi huu ambapo
kiasi kinachotakiwa ni sh 8,000,000 ilikuweza kufanikisha maandalizi yote ya
kongamano hilo ambalo litashirikisha vijana wa vyuo vikuu 600.
0 comments:
Chapisha Maoni