Searching...
Jumatano, 3 Julai 2013

MKE WA RC RUVUMA AHIMIZA UPENDO BAINA YA WANAWAKE KWA WANAWAKE

Mama Anabu Mwambungu Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

 Na Joyce Joliga,
WANAWAKE mkoani Ruvuma wameshauriwa kupendana, kushirikiana na kuacha tabia ya kusengenyana ili waweze kufanikiwa kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali ili viweze kuwasaidia kuinua kipato chao na familia zao na wasikubali kugombanishwa .
 Picha wadau wakiwa katika hatua ya mwisho katika uvunaji wa mahindi
Ushauri huo umetolewa jana na Mke wa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakati akizindua rasmi kikundi cha wanawake wajasilimali  wanaojishugulisha na ufugaji wa kuku wa nyama na mayai cha JITIHADA GROUP kilichopo kata ya Lizabon Manispaa ya Songea.
Amesema,ili wanawake waweze kufanikiwa kimaendeleo wanapaswa kujenga moyo wa kupendana kwa dhati , kuaminiana na kushirikiana  na kuacha tabia ya kupigana majungu kitu  ambacho kimekuwa kikiua vikundi vingi vya wanawake .
Anabu ameongeza kuwa ,wanawake  wengi wamekuwa wakifanikiwa kuanzisha vikundi  ila vimekuwa havifiki mbali na kuvunjika kitu ambacho si kizuri hivyo amewataka wanawake kuwa makini na miradi wanayoaanzisha ikiwa ni pamoja na kushikamana ili waweze kujiletea maendeleo.
“Nawashauri wanawake wenzangu ,kikundi hiki tukiendeleze ili kiweze kutusaidia kujikwamua na umaskini kamwe tusikubali kugambanishwa na vijimajungu vidogo vidogo ,kwani  hiyo ndiyo sumu ya vikundi vingi ,mpendane, muaminiane ,mshirikiane na kuvumiliana na mtafika mbali , name nawaunga mkono nawachangia kiasi cha sh 200,000,”alisema Anabu Mwambungu.
Awali akisoma taarifa ya kikundi hicho Katibu wa Kikundi hicho Theresia Komba amesema,bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na kukosa mtaji  hali inayowafanya washindwe kuzalisha kwa wingi,pamoja na ukosefu wa elimu ya ujasiliamali hususani wa ufugaji bora.
Aidha, wamemwomba Mke wa Mkuu wa mkoa kuwasaidia ili waweze kupata mkopo pamoja na pembejeo za kilimo ili waweze kuzalisha kwa wingi na kujiongezea kipato.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!