Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiongoza wananchi mbali mbali walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort jana.

Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort jana,akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bibi Mizinga Mellu,(wa pili kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi Mwanaidi (kulia) .


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania,Bibi Mizinga Mellu,akizungumza machache na kutoa salamu za Uongozi wa Benki hiyo wakati wa futari waliyoiandaa kwa wananchi wa Zanzibar jana katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,Wilaya ya Magharibi Unguja.



Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi,akisoma Dua baada ya kumalizika kwa futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort jana,kwa Wananchi wa mbali mbali na wateja wa Benki hiyo upande wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamohamed Shein,(kushoto) akisindikizwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Bibi Mizinga Mellu,baada ya kumalizika kwa futari iliyoandaliwa na Benki hiyo jana katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort nje ya Mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamohamed Shein,(kushoto)akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Bibi Mizinga Mellu,(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,(kati) baada ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo jana katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort nje ya Mji wa Unguja.
[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.