Searching...
Jumapili, 21 Julai 2013

NATAKA KUJIUNGA NA MOURINHO-ROONEY

Wayne Rooney in a Chelsea Shirt 
WAYNE ROONEY-MCHEZAJI WA MAN UNITED.
...Ule usemi usemao mla huliwa ndio unaoendelea kudhihirika hivi sasa katika usajili wa wasukuma ndinga au soka barani Ulaya baada ya Man U kutangaza dau la kufuru kwa Barcelona kumng'oa Cesc Fabregas Chelsea nao wamepanda dau la kufuru kwa kutaka kumng'oa Rooney Old Trafod msimu huu.
Imefahamika wazi kwamba sasa Rooney yupo karibu kumwaga wino Chelsea msimu huu kutokana na kauli yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari kwamba sio tu kwamba na taka kuondoka Man U bali anatarajia kutimiza ndoto yake ya kuwa chini ya mreno mwenye mbwembwe Jose Mourinho
"Sio tu kwamba nimechanganyikiwa na hali ya maisha yangu hapa Manchester United,bali ninataka kujiunga na Mourinho Stamford Bridge  ili kutimiza ndoto zangu za muda mrefu..."alikaririwa Rooney.
 FBL-ASIA-ENG-PR-AUS-MANUTD
DAVID MOYES - KOCHA MAN U.
Kocha wa Man U David Moyes pamoja na viongozi wa klabu akiwemo makamu mwenyekiti Ed Woodward, wameendelea kusisitiza kwamba Rooney hauzwi lakini Chelsea wao wameendelea kujaribu bahati yao baada ya kutuma ofa mpya ya paundi milioni 40 ili kumnasa mshambuliaji huyo wa kimataifa Wayne Rooney ambaye hana raha na maisha pale Unite.
Absence: Alex Ferguson is missing Murray's final to go on a cruise ship around the Scottish Islands
SIR ALEX FERGUSON-KOCHA WA ZAMANI WA MAN U.
Rooney bado ana hasira na kauli iliyowahi kutolewa na kocha wake wa zamani Ferguson kwamba alimuambia anataka kuondoka klabuni hapo katika kikao chao cha siri kilichofanyika mwezi wa nne mwaka jana kauli ambayo Rooney ameikanusha vikali na kumtaka Moyes kama anataka abaki aweke wazi kwamba mzee Ferguson alitoa kauli ya uongo kwa Rooney kitendo ambacho klabu ya Man U wanaona kufanya hivyo ni kumdhalilisha Babu Ferguson mwenye heshima kubwa katika klabu hiyo.
 Chelsea magazine
JOSE MOURINHO-KOCHA CHELSEA.
Rooney ni chaguo namba moja la Mourinho katika msimu huu wa usajili ambapo Chelsea wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kupitia hali ya kutoelewana kati ya Rooney na Moyes basi wanatumia mwanya huo kupata saini ya mfumania nyavu huyo wa kimataifa wa England na sasa wametuma ofa ya ada ya uhamisho ya paundi milioni 40.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!