Searching...
Jumapili, 21 Julai 2013

MANCHESTER UNITED YAINYONG'ONYEZA BARCELONA-KUMLIPA FABREGAS MSHAHARA MARA MBILI YA BARCELONA

United target Fabregas after Thiago snubCESC FABREGAS - MCHEZAJI BARCELONA.
Katika hali ya kuonyesha kwamba Man U wamepania kumsajili Febregas kutoka Barcelona msimu huu,sasa Manchester United wametangaza ofa kwa mchezaji kwamba endapo atakubali kujiunga na mashetani hao wekundu atalipwa mshara mara mbili ya ule anaolipwa sasa hivi kule Noucamp ambapo kwa sasa analipwa paundi laki moja kwa wiki kitendo ambacho kama atakubali kwenda Man U basi atalipwa kitita cha paundi laki mbili kwa wiki ofa ambayo imetafsiriwa kwamba ni vigumu sana Cesc kuikataa ukilinganisha pia na ugumu wa kucheza kikosi namba moja Barcelona.A-League All-Stars v Manchester United
DAVID MOYES-KOCHA MAN U
Kocha David Moyes anajiandaa kuvunja benk kwa kuweka historia baada ya kutuma ofa mpya ya uhamisho kwa Barcelona ya kitita cha paundi milioni 30 ikiwa ni pamoja na kumlipa mchezaji huyo mara mbili ya mshahara wake wa sasa pale Noucamp. 
Mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo ambaye anatakiwa na Man U ili kuchukua nafasi ya kiungo mkongwe aliyestaafu Paul ­Scholes sasa anasubiri kusikia kutoka kwa uongozi wa klabu yake kama watakubali ofa hiyo au la,mkataba wa Fabregas Barcelona unaisha mwaka 2016.
Chanzo cha habari kutoka nchini Hispania kinasema Man U wamekufa wameoza kwa kiuongo huyo wa kimataifa wa Hispania na wameapa kufa kupona kupata saini yake msimu huu wa usajili,hata hivyo mchezaji huyo aliwahi kuwaambia marafiki zake kwamba kama atarejea ligi kuu England basi ni Arsenal na sio timu nyingine lakini kwa kitita hicho bila shaka atabadili mawazo na msimamo wake

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!