Hayawi hayawi sasa yanawadia baada ya mashetani wekundu Man U kumrushia ndoano mara kadhaa sasa baada ya kumhakikishia Mchezaji wa Barcelena na timu ya taifa ya Hispania Cesc Fabregas kwamba atalipwa mshara mara mbili ya ule anaolipwa pale Barcelona yaani paundi laki mbili kwa wiki badala ya paundi laki moja anayolipwa sasa hatimaye sasa amewaambia marafiki zake kwamba anataka kujiunga na klabu ya Manchester United msimu huu wa uhamisho....Chezea hela weweee!!!!
Man United tayari wameshakwaa kisiki kwa nahodha wa zamani wa Arsenal Fabregas ambaye ndio chaguo lao la kwanza katika uhamisho msimu huu,mara ya kwanza walituma ofa ya ada ya uhamisho ya paundi milioni 26,mara ya pili paundi milioni 29 na mara ya tatu paundi milioni 30.
DAVID MOYES
Akizungummza kwa kujiamini kocha wa Man U David Moyes amesema anayo matumaini makubwa kumnyakua mhispania huyo Cesc Fabregas.
Fabregas hachukuliwi kama mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza the Nou Camp na hii inamaanisha kwamba kama United wataenda na hela inayoridhisha basi ni dhahiri kwamba watampata mmoja kati ya viungo bora duniani kwa sasa
Tayari Moyes ameshaandaa mbadala wa Fabregas kama watashindwa kumpata na chaguo lao ni mchezaji kiungo wa Borussia Dortmund ace Ilkay Gundogan ambaye pia itakua shughuli kumng'oa panapo klabu hiyo ya ujerumani.
‘Dili la uhamisho wa Fabregas bado linaendelea, bado tuna matumaini,’ alisema Moyes. ‘lakini siwezi nikawaambia kingine chochote zaidi ya hilo.’
mkataba wa Fabregas panapo klabu yake ya Barcelona unaisha mwaka 2016 ambapo klabu yake ya zamani ya Arsenal walitarajia kumsajili msimu huu lakini mipango yao inaonekana ni butu zaidi na hivyo kuishia kutazama.
0 comments:
Chapisha Maoni