JOSE MOURINHO-KOCHA CHELSEA.
Jose Mourinho amesema kwamba klabu ya Chelsea walikua hawajulikani katika ramani ya soka duniani kabla hajaenda kuifundisha klabu hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2004 ambapo alifanya kazi kubwa kuiweka kwenye ramani ya soka duniani.
Mourinho amesema kwa sasa malengo yake ni kuijenga zaidi klabu hiyo na kuzipiku klabu za Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich na Manchester United.
ameongeza kuwa uteuzi wake kuifundisha
klabu hiyo mwaka 2004 aliweza kuleta ushindani mkubwa kwa kipindi chote alipokuwa hapo darajani ambapo aliweza kukusanya vikombe 11 ukilinganisha na vikombe 9 walivyojichukulia Manchester United
Mourinho anaanza rasmi kibarua cha kuinoa Chelsea
kwa mara ya pili kesho kabla ya kwenda Asia katika mechi za maandalizi ya msimu wa ligi ujao,taarifa zinasema Chelsea wataweka kambi Bangkok, Kuala Lumpur na Jakarta
“Kwa mara ya kwanza nilivyoanza kuifundisha timu hii mwaka 2004 tulikwenda kuweka kambi Marekani kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi nilikua na watoto 10” alisema
Mourinho.
“Hakuna mtu aliyekuwa amatushobokea tulipokuwa tunapita mitaani,nakumbuka kuna mtu aliwahi kusema oooooh umemuona Frank Lampard’lakini sio wengine.
“baada ya miaka miwili mwaka 2006 tulishinda vikombe na mmiliki akaanza kununua wachezaji wakubwa baada ya kushinda kombe la ligi kuu na kufika nusu fainali ya klabu bingwa ulaya mambo yakaanza kubadilika.
“Tulirejea tena Marekani,wakati huu mambo yakawa tofauti kabisa kwani watu takribani alfu tatu au alfu nne walikuwa wakiangalia mazoezi yetu na mechi mbalimbali tulizokuwa tunacheza pale Los Angeles.
“Lakini ukweli ni kwamba historia ya klabu hii ya Chelsea katika kipindi cha miaka kumi ni kwamba Chelsea wameshinda vikombe vingi kuliko Manchester United...Alijigamba Mourinho

0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.