Rais mpya wa Misri ameanza kuimarisha madaraka yake na udhibiti wa mitaa
hata wakati wapinzani wake wa chama cha Kiislamu wakisema kuwa mamlaka
yake ni kinyume na sheria na wakidai rais Mursi arejeshwe madarakani.
Kuondolewa kwa Morsi madarakani kwa njia ya mapinduzi kumesababisha
maandamano makubwa pamoja na mapambano ya mitaani kati ya makundi
hasimu.
ELBaradei hatakiwi
Kuonesha hali ya mgawanyiko mkubwa unaomkabili kiongozi huyo asiye na
uzoefu wa kutosha , Adly Mansour, ofisi yake imesema kuwa kiongozi
anayependelea mageuzi Mohammed ElBaradei ameteuliwa kuwa waziri mkuu wa
mpito lakini kauli hiyo ilibadilishwa haraka baadaye na kusema kuwa
mashauriano bado yanaendelea .
Mwanasiasa ambaye yuko karibu na ElBaradei amesema hatua hiyo ya
kubadilisha uamuzi inatokana na upinzani kutoka kwa chama cha
kihafidhina kinachofuata siasa kali zinazoegemea dini ya Kiislamu
ambacho utawala mpya unataka kushirikiana nacho.
Utawala wa Mansour , wakati huo huo , umeanza kujaribu kuondoa kile
Morsi alichokijenga. Amemuondoa mkuu wa usalama wa taifa na mnadhimu
mkuu wa ikulu ya nchi hiyo.
Hakuna ghasia kubwa zilizoripotiwa kati ya waungaji mkono na wapinzani wa Morsi wakati pande hizo mbili zimejikusanya tena baada ya usiku wa mapambano makali ambayo yameufanya mji wa Cairo kuwa eneo la mapambano.
Mapigano pia yamekuwa makali katika mji wa bandari wa Alexandria, ambako maelfu ya wafuasia wa kila upande walipigana kwa risasi, mabomu ya moto na virungu.
Ghasia za Ijumaa zimesababisha watu 36 kuuwawa, na kufikisha idadi ya karibu watu 75 waliouwawa tangu ghasia hizo kuzuka hapo Juni 30, wakati mamilioni ya waandamanaji wakiingia mitaani katika mkesha wa mwaka wa kwanza tangu Morsi kuingia madarakani kidemokrasia.
Morsi ambaye ni mhandisi aliyepata mafunzo yake nchini Marekani ambaye anashutumiwa sana na wakosoaji kwa kuhodhi madaraka binafsi na kwa ajili ya chama chake cha udugu wa Kiislamu pamoja na kushindwa kwake kutekeleza mageuzi ya kidemokrasia ya kiuchumi , ameendelea kubaki kizuwizini katika eneo ambalo halijilikani.
Jenerali huyo wa jeshi amekana kuwa amefanya mapinduzi ya jeshi, akisema kuwa alikuwa anachukua hatua za matakwa ya mamilioni ya Wamisri wanaoandamana dhidi ya rais huyo wa zamani.
Mwandishi : Sekione Kitojo / ape / dpae
Viongozi wabaki korokoroni
Waendesha mashtaka, wakati huo huo , wameamuru viongozi wakuu wa chama
cha Morsi cha udugu wa Kiislamu ambao wamewekwa kizuizini washikiliwe
kwa muda wa siku 15 wakisubiri uchunguzi uendelee kuhusiana na
kushambuliwa na kuuwawa kwa waandamanaji wanane wiki iliyopita.Hakuna ghasia kubwa zilizoripotiwa kati ya waungaji mkono na wapinzani wa Morsi wakati pande hizo mbili zimejikusanya tena baada ya usiku wa mapambano makali ambayo yameufanya mji wa Cairo kuwa eneo la mapambano.
Mapigano pia yamekuwa makali katika mji wa bandari wa Alexandria, ambako maelfu ya wafuasia wa kila upande walipigana kwa risasi, mabomu ya moto na virungu.
Ghasia za Ijumaa zimesababisha watu 36 kuuwawa, na kufikisha idadi ya karibu watu 75 waliouwawa tangu ghasia hizo kuzuka hapo Juni 30, wakati mamilioni ya waandamanaji wakiingia mitaani katika mkesha wa mwaka wa kwanza tangu Morsi kuingia madarakani kidemokrasia.
Morsi ambaye ni mhandisi aliyepata mafunzo yake nchini Marekani ambaye anashutumiwa sana na wakosoaji kwa kuhodhi madaraka binafsi na kwa ajili ya chama chake cha udugu wa Kiislamu pamoja na kushindwa kwake kutekeleza mageuzi ya kidemokrasia ya kiuchumi , ameendelea kubaki kizuwizini katika eneo ambalo halijilikani.
Wasi wasi wazidi
Hali ya wasiwasi imeendelea kuongezeka wakati mamia kwa maelfu ya
wafuasia wa Morsi wakiingia mitaani kwa siku ya tatu karibu na msikiti
katika eneo la mji wa Cairo ambalo kwa kawaida ni ngome kuu ya chama
chake, wakiimba kauli mbiu za hasira dhidi ya kile wanachokiita
mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na jenerali wa jeshi Abdel-Fattah
el-Sissi.Jenerali huyo wa jeshi amekana kuwa amefanya mapinduzi ya jeshi, akisema kuwa alikuwa anachukua hatua za matakwa ya mamilioni ya Wamisri wanaoandamana dhidi ya rais huyo wa zamani.
Mwandishi : Sekione Kitojo / ape / dpae
Mhariri: Amina Aboubakar
0 comments:
Chapisha Maoni