Searching...
Ijumaa, 12 Julai 2013

MKENYA VICTOR WANYAMA ATUA RASMI ENGLAND AVUNJA REKODI

New boy: Mauricio Pochettino welcomes Victor Wanyama to the SaintsVICTOR WANYAMA AKIKABIDHIWA JEZI SOUTHAMPTON.
klabu ya Southampton ya England imemsajili kiungo wa klabu ya Celtic mkenya Victor Wanyama kwa kitita cha paundi milioni12.5.
mkenya huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye alijiunga na Celtic akitokea klabu ya Ubelgiji ya Beerschot kwa ada ya uhamisho ya paundi 900,000 miaka miwili iliyopita amekubali kuingia mkataba wa miaka minne na Southanpton ya England na kuweka historia ya mchezaji wa kwanza kutoka afrika mashariki kucheza ligi kuu ya England.
Mkenya huyo Wanyama aliwahi kuwa mchezaji bora  mdogo wa mwaka kwa ligi kuu ya Scotland msimu uliopita na kufunga goli safi la kicha katika mechi ya klabu bingwa ulaya dhidi ya Barcelona na kuvunja rekodi ya klabu yake kuwahi kutokea kwa kupokea kitita kikubwa kwa kumuuza mkenya huyo.
Moving south: Wanyama will join the south coast side despite interest from Cardiff
VICTOR WANYAMANDANI YA JEZI YA SOUTHAMPTON
 Southampton ni timu borana ina wachezaji bora,kwahiyo najivunia kuwa hapa na ninachokitaka ni kufanya kila niliwezalo kwa juhudi na maarifa ili kuwa katika wachezaji bora kumi na mmoja wa kwanza”amekaririwa Victor Wanyama

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!