Searching...
Jumanne, 2 Julai 2013

LEO HAKUNA USAFIRI WA TREN JIJINI DAR ES SALAAM,ILI KUPISHA ZIARA YA OBAMA



Jana mnamo saa 11:30 asubuhi vichwa viwili vya treni ya huduma la jiji la Dar es Salaam vilipata ajali ya kugongwa na roli la mizigo aina ya Fusso katika makutano ya reli na barabara ya Kawawa jijini Dar es salaam , katika ajali hiyo dereva wa Fusso alifariki duniani papohapo hata hivyo Utingo wake alinusurika.

Hata hivyo vichwa hivyo vya treni vilipata mkosi tena wa ajali ambapo viligongwa na basi dogo la Daladala aina ya Isuzu katika makutano ya reli eneo la Kamata. Tukio hilo lilisababisha majeruhi kadhaa katika basi hilo la daladala ambapo majeruhi  wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwemo askari wawili Polisi kutoka Kikosi cha Reli  mmojawapo akiwa  mahututi.
Vichwa hivyo viifanikiwa kufika steshesheni kwa wakati na kuanza kutoa huduma ya usafiri wa treni jijini  kutoka Dar Stesheni kwenda Ubungo Maziwa hadi saa 5 asubuhi hata hivyo huduma ya jana  jioni Julai 01, 2013, ilisogezwa mbele na kutarajiwa kuanza saa 12 jioni badala ya saa 10:30 alasiri. 

mabadiliko haya yamebidi yafanyike   kufuatia Jiji la Dar es Salaam kuwa na hekaheka ya kumpokea Raisi wa Marekani Barack Obama.
Aidha uongozi wa  TRL unawataarifu wakazi wa jiji kuwa leo Julai 02, 2013, huduma za treni ya jiji hazitakuwepo hadi kesho Julai 03, 2013, ambapo zitaendelea kama kawaida.
Imtolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
 Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.
Makao Makuu ya TRL
Dar es Salaam.
Julai 01, 2013.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!