Searching...
Ijumaa, 12 Julai 2013

ILE SINEMA YA ROONEY BADO INAENDELEA-AACHANA NA TIMU ASEMA AMEUMUA AREJEA NYUMBANI AENDELEA NA MSIMAMO WAKE-NATAKA KUONDOKA MAN U.

 Uncertainty: Wayne Rooney's future is still up in the air despite his return to training
WAYNE ROONEY 

Taarifa kutoka kwenye gazeti la leo ijumaa la DAILY STAR zinasema bado Mchezaji huyo wa kimataifa wa England Wayne Rooney anataka kuondoka klabuni hapo na kumfanya Mourinho kujiaminisha kwamba anaweza kuinasa saini ya mfumania nyavu huyo wa Mahasimu wao Man kwa kitita cha paundi milioni 25.
Kocha wa Manchester United David Moyes alithibitisha kwamba amekutana na Rooney mara tatu au nne kujadili muafaka wake ndani ya mabingwa hao wa England na kusisitiza kwamba mchezaji huyo hauzwi.
Moyes amezidi kuchanganyikiwa zaidi baada ya msukuma ndinga huyo anayelipwa paundi 240,000 kwa wiki kuumia na kurejea nyumbani na kuiacha timu ikiendelea na maandalizi ya msimu ujao wa soka.
David Moyes amesema malengo yake yalikua ni kutumia wiki tatu za maandalizi ya msimu ujao kutumia muda mwingi kumshauri na kumshawishi Rooney kuendelea kukipiga Old Trafford lakini matumaini yake yamepotea baada ya mchezaji huyo kuumia na kuweka wazi kwamba anarejea nyumbani kwaajili ya matibabu
Taarifa zinasema atakua nje kwa muda wa mwezi mmoja na hivyo atakosa mechi ya ufunguzi wa ligi dhidi ya Swansea na mechi ya kimataifa kati ya England dhidi ya Scotland.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!