Kocha wa Manchester United David Moyes yupo njiani kurejea England baada ya ziara yao ya maandalizi ya msimu ujao ambapo ameweka wazi kwamba anaandaa mazungumzo na mshambuliaji wake Wayne Rooney kwaajili ya mustakabali wake msimu ujao.
Wawili hao hawajawahi kuongea tangu Moyes atoe kauli iliyomuudhi Rooney kwamba anahitaji Rooney aendelee kukipiga Man U kama mchezaji wa akiba akimsubiri Robin van Persie aumie ndio acheze.
KARIBUNI NYUMBANI: David Moyes na timu yake wakiwasili klabuni kwao Manchester leo jumanne wakitokea Hong Kong walipokuwa kwenye ziara ya maandalizi ya msimu ujao.
NAJIACHIA: Rooney akiwa katika hali ya kujiachia akila bata na mkewe kwenye fukwe moja huko nchini Ureno wakati wenzake wakiwa Hong Kong
Moyes na timu yake wametua Manchester mapema leo jumanne asubuhi wakitokea Hong Kong baada ya kumaliza ziara yao nchini
Australia na mashariki ya mbali wakiwa hawajamuona Rooney kwa takribani wiki tatu tangu alipoondoka kambini Bangkok kutokana na majeruhi.Rooney alitarajiwa kurejea uwanjani kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya AIK huko Stockhol.
Rooney ameonekana akila bata huko ureno japo inafahamika kwamba anayo ruhusa rasmi ya timu yake lakini Moyes baada ya ushindi wa 5-2 dhidi ya Kitchee FC Hong Kong amekaririwa akisema kwamba hakuna mazungumzo yoyote kati ya Chelsea na Man U kuhusu Rooney tangu United wakatae ofa ya paundi milioni 20 mapema mwezi huu.
Wayne Rooney akila bata na mkewe huko Ureno.
Tule maisha mama-Rooney
Moyes na dawati lake la ufundi wakiwa ziarani mashariki ya mbali
0 comments:
Chapisha Maoni