MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center
(HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali
maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika
Kusini kwa matibabu zaidi .
Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa
tindikali na mtu mmoja ambaye........
hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.
Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki.
Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua. Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.
Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake

HABARI NA KILIMANJARO OFFICIAL WEBSITE
0 comments:
Chapisha Maoni