Mtaalamu
wa Viwango wa kampuni ya Tigo Pamela Shelukindo (kushoto) akizungumzia
kuzinduliwa kwa huduma ya ‘News SMS Service’ ambayo inalenga kuwapa
habari wateja wa Mtandao wa Tigo popote pale walipo. Amesema huduma hiyo
itakayokuwa ikipatikana kwa kutuma neon ‘GUARDIAN SMS na NIPASHE SMS
itakuwa ikisimamiwa kiufundi na kampuni ya Premier Mobile Solutions
(PMS). Katikati ni Meneja Mipango Msaidizi wa kampuni ya Premier Mobile
Solutions Bi. Lulu Ramole na kulia ni Meneja Masoko Msaidizi Emmanuel
Matondo.
Meneja
Mipango Msaidizi wa kampuni ya Premier Mobile Solutions Bi. Lulu Ramole
(kulia) akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema huduma hiyo
ya ujumbe wa habari kwa maandishi imetengenezwa kuwawezesha wateja
kupata habari mara moja ambapo watumiaji wa mtandao wa Tigo watachajiwa
mara moja kwa siku na kuweza kupata vichwa vya habari mara nne (4).
Meneja
Masoko wa Guardian Simon Marwa akifafanua kuwa ubunifu wa huduma ya
habari kwa njia ya ujumbe wa maandishi katika simu ya mkononi bila shaka
utawawezesha wasomaji wa magazeti ya ‘The Guardian’ na ‘Nipashe’ ambao
pia ni watumiaji wa mtandao wa Tigo kupata habari mpya za uhakika
kupitia simu zao za mkononi.
0 comments:
Chapisha Maoni