JOHN TERRY NA JOSE MOURINHO.
Pamoja na kusaliwa na mkataba wa mwaka mmoja Nahodha wa klabu ya Chelsea muingereza John Terry amekataa kuongeza mkataba na klabu hiyo kwa masharti ya kumtaka kocha mpya Jose Mourinho kumhakikishia nafasi yake ya kucheza kutokana na kocha huyo kuonekana kuwa na mipango ya kuijenga upya timu hiyo huku Mourinho akionekana kuwa na mipango ya kumsajili beki kisiki wa Porto anaitwa MANGALA (pichani chini) kitendo ambacho kimemtisha Terry kwamba huenda akakalia benchi.
CARLOS TERVEZ AKIWA SALOON.
Juventus wameamua kuhamishia juhudi zao kumsajili Carlos Tervez mshambuliaji wa Manchester City ambaye amebakisha mkataba wa mwaka mmoja baada ya kushindwa kupanda dau la kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina Stevan Jovetic (pichani chini)ambaye pia anawaniwa na vilabu vya Chelsea na Arsenal.
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.