Searching...
Jumatatu, 1 Julai 2013

TETESI ZA UHAMISHO WA WACHEZA SOKA ULAYA,NATAKA KUCHEZA NA ROONEY BARCELONA-NEYMAR

Brazil's forward Neymar celebrates after scoring against Italy during their FIFA Confederations Cup Brazil 2013 Group A football match, at the Fonte Nova Arena in Salvador, on June 22, 2013. AFP PHOTO / CHRISTOPHE SIMONCHRISTOPHE SIMON/AFP/Getty Images
NEYMAR DA SILVA SANTOS JUNIOR.
Mchezaji mpya chipukizi wa klabu ya Barcelona mbrazili Neymar ameweka wazi na kuutaka uongozi wa Barcelona kufanya kila linalowezekana kumsajili mshambuliaji nguli wa Manchester United Wayne Rooney ili waweze kutengeneza safu ya ushambuliaji ya kutisha duniani hapo msimu ujao.
Hatma ya Rooney ndani ya klabu yake ya Manchester United ipo mikononi mwa kocha mpya wa klabu hiyo Moyes baada ya msuguano uliojitokeza baina ya Rooney na Sir Alex Ferguson ambaye alisema Rooney hataki kuichezea klabu hiyo kauli ambayo Rooney ameikanusha vikali na kumtaka Moyes kuiambia dunia kwamba hiyo ilikua kauli ya Ferguson na sio Rooney bila hivyo anaondoka klabuni hapo msimu ujao
Vilabu vya Chelsea na Arsenal tayari wameonyesha nia ya kumnyakua Rooney lakini sasa kauli ya Neymar imemuongezea nguvu Rooney kujiunga na miamba hiyo ya soka ya Spain ili kuungana na Neymar pamoja na Messi
 And smile he might: Garay has edged closer to his dream United move
EZEKIEL GARAY.
Kocha wa Manchester United David Moyes anaanza kazi rasmi leo Old Trafod na yupo tayari kumsainisha kiungo wa timu ya Benfica muagentina Ezeguiel Garay.
Klabu hiyo ya ureno imesema ipo tayari kumuuza kiungo huyo kwasababu tayari wameshamsajili mchezaji mbadala wake kutoka Arsenal De Sarandi ambaye pia ni muagentina mwenzake Lisandro Ezequiel Lopez. David Luiz and Paulinho: Chelsea defender has backed Brazil midfielder to shine in the Premier League
DAVID LUIZ na PAULINHO.
Beki wa Chelsea mbrazili David Luiz amemtabiria mbrazili mwenzake Paulinho kwamba atang'ara katika ligi kuu England kama ataamua kuhamia huko msimu ujao.

"Kama Paulinho atakwenda kucheza soka England,kwa hakika atakwenda mbali sana", Luiz aliuambia mtandao wa Fifa.com.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!