Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu akizungumza katika kikao cha
uvunjaji wa baraza la madiwani wa wilaya ya Mbinga leo hii katika ukumbi
wa Maendeleo.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu akionyesha hati za utambulisho
wa Halmashauri mbili za nyasa na mbinga kabla yta kukabidhi hati hizo
Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyasa Shaib Mnunduma akipokea hati ya utambulisho wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa
Toka toka kushoto kwako aliyekaa ni mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga
na aliyesimama ni Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga
Hussen Ngaga
akizungumza jambo wakati wa Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kabla
ya kuvunjwa.
Mkuu wa wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi akizungumza baada ya kutangazwa
na mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwangu kuvunjwa Baraza la
madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga
Baadhi ya wataalam wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga na Nyasa
wakisikiliza nasaha za viongozi Mbalimbali kabla ya kuvunjwa kwa Baraza
la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga kufuatia kuzaliwa kwa
Halmashauri mpya ya Nyasa.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambayo
imezaa Halmashauri mpya ya Nyasa wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Said Thabiti Mwambungu alipokuwa akitoa nasaha zake wakati wa uvunjaji wa Balaza la madiwani.
-----------------------------------------
Na Nathan Mtega,Mbinga
HATIMAYE baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya
Mbinga mkoani Ruvumalimegawanyika baada ya mchakato wa kuanzishwa kwa halmashauri
mpya ya wilaya ya Nyasa na kupatikana kwa wakurugenzi wa halmashauri hizo mbili
na kukabidhiwa hati za utambulisho wa halmashauri zilizokabidhiwa kwa
wakurugenzi wa halmashauri hizo na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu baada
ya kuvunjwa kwa baraza hilo.
Akizingumza katika kikao hicho cha dharula cha baraza la
madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said
Mwambungu mbali ya kulipongeza baraza hilo la madiwani lililokuwa linagawinyika
kwa ajili ya kuanzishwa kwa baraza jipya la halmashauri ya wilaya ya Nyasa
amesema kuwa maendeleo na mafanikio makubwa yaliyopo katika halmashauriya
wilaya ya Mbinga yametokana na ushirikiano uliokuwepo baina ya madiwani hao
pamoja na wataalamu hivyo unapaswa kuendelezwa kwa pande zote mbili.
Amesema mgawanyiko huo unapaswa kuwa kichocheo cha maendeleo
ya kwa pande hizo mbili ambazo zimegawanyika kwa kufuata kanuni na sheria
zilizopo bila kutokea hitilafu yoyote katika mgawanyo wa mali, watumishi pamoja
naadeni yaliyopo hali inaonyesha ukomavu wa viongozi pamoja na wataalamu wao
ambao kwa pamoja waliifanya halmashauri ya wilaya ya Mbinga kuwa na sifa kubwa
ya uzalishaji na ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Aidha amewataka wakurugenzi watendaji wa halmashauri hizo
mbili kuhakikisha watumishi waliopangwa kwenye halmashauri hizo baada ya mgawanyo
huo kuwa wameripoti kwenye vituo vyao
vya kazi ifikapo Julai mosi mwaka huu bila kuwepo kwa visingizio vya aina
yoyote kwa sababu wanapaswa kuheshimu mabadiliko hayo yaliyofuata taratibu na
kupewa baraka na uchaguzi wa wenyeviti na viongozi wengine kwenye halmashauri
hizo unapaswa kuwa umefanyika katika kipindi hicho bila kutokea vurugu yoyote.
Alisema kuwa halmashauri ya wilaya ya Mbinga imekuwa ikipata
hati safi ikiwa na baraza la madiwani 48
kablaya mgawanyo huo na hati hizo zilipatikana kwa ushirikianomzuri uliokuwepo
hivyo hati safi hizo zitaendelea kwa pande zote mbili ambazo awali zilikuwa
pamoja na ushirikiano unapaswa kudumishwa kwa ajili ya maslahi na maendeleo ya
wananchi wa halmashauri hizo.
Amesema kuwa serikali kuu itatoa ushirikiano wa karibu kwa
halmashauri mpya ya Nyasa ili kuhakikisha inapiga hatua kimaendeleo na kuweza
kutoa huduma bora kwa wananchi huku akiwataka wakururugenzi wa halmashauri hizo
Shaib Mnunduma(Nyasa) na Hussein Issa(Mbinga) kuendelea kutoa ushirikiano kwa
madiwani.
Wakizungumza baada ya mkuu wa mkoa wabunge wawili wa wilaya
hizo mbili Kapten John Komba na Gaudens Kayombo mbali ya kupongeza uamuzi wa serikali
kukubali ombo lao hilo la muda mrefu la kuwepo kwa mgawanyo wa wilaya na
halmashauri lakini pia waliwataka madiwani na wataalamu kwenye halmashauri hizo
kuendeleza ushirikiano wa karibu uliokuwepo kwa ajili ya maslahi ya wananchi
wanaowaongoza.
Aidha nao wakuu wa wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi wa Nyasa
na Senyi Ngaga wa Mbinga kwa pamoja
walishauri kuwepo kwa ushindani wa kimaendeleo kw ajili ya wananchi na si vinginevyo
kwa sababu wilaya ya Mbinga haina utamaduni wa migogoro inayorudisha nyuma jitihada
za wananchi katika kujiletea maendeleo yao.
HABARI KWA HISANI YA DEMASHO BLOG.
HABARI KWA HISANI YA DEMASHO BLOG.
0 comments:
Chapisha Maoni