Na Edwin Moshi
Imeelezwa kuwa wanaume waliofanyiwa
tohara si kweli kwamba hawatapata virusi vya Ukimwi na badala yake
kutawasaidia kupunguza uwezekano wa kupata vvu kwa asilimia 60
Hayo
yamesemwa na mratibu wa Ukimwi wilaya ya Makete(DAC) Dkt. Shadrack
Sanga(pichani) wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu umuhimu wa
tohara ya wanaume wilayani hapo
Amesema
kumekuwa na taarifa zilizozagaa kuwa mwanaume akishafanyiwa tohara
hawezi kupata vvu ambapoa amesema taarifa hizo si za kweli na ukweli ni
kwamba mwanaume huyo atapunguza asilimia 60 za kupata vvu kuliko yule
ambaye hajatahiriwa
"Naomba
hili lieleweke wazi, mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara na yule
aliyefanyiwa wote wanaweza kupata vvu, lakini aliyefanyiwa tohara
anaupungufu wa asilimia 60 kupata vvu lakini si kwamba hatapata" alisema
Katika
hatua nyingine Dkt. Sanga amesema tangu kampeni ya tohara ya wanaume
maarufu kama dondosha mkono sweta ianze rasmi wilayani Makete mwaka 2011
jumla ya wanaume 9,669 wamefanyiwa tohara
Amesema
muitikio ni mzuri lakini bado idadi ya wanaume ambao hawajafanyiwa
tohara ni kubwa hivyo anatoa wito kwa wanaume kuacha woga na aibu ya
kwenda kufanyiwa tohara ambayo ianatolewa bure
Hivi
sasa mkoa wa Njombe unaongoza kitaifa kwa kuwa na maambukizi makubwa ya
virusi vya Ukimwi, ambapo imegundulika kuwa wanaume wengi wa mkoa huo
kutofanyiwa tohara ni miongoni mwa sababu kubwa zinazopelekea maambukizi
hayo kuwa juu
0 comments:
Chapisha Maoni