SEHEMU YA BAADHI YA WANAFUNZI WAKIWA WAMEKAA CHINI ILI KUPOKEA MADAWATI HAYO
MKUU WA MKOA WA MWANZA ENG.EVARIST NDIKILO AKIZUNGUMZA WAKATI WA HAFLA YA KUPOKEA MADAWATI HAYO KUTOKA TAASISI YA HASSAN MAAJAR TRUST JIJINI MWANZA.
WANAFUNZI WAKIFURAHIA MADAWATI WALIYOPEWA MSAADA NA HMT.
KAULI MBIU YA HMT...KILA MTOTO ANAYO HAKI YA KUKAA KWENYE DAWATI.
Bwana Shariff Maajar, pamoja na
Bi Zena M Tenga kwa niaba ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust wakikabidhi
madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Engineer Evaristi Ndikilo.
SEHEMU YA JUMLA YA MADAWATI 250 YALIYOTOLEWA NA TAASISI YA HASSAN MAAJAR TRUST HMT KWA SHULE TANO ZA WILAYA TANO MKOANI MWANZA
Taarifa
Kwa Vyombo Vya Habari
Taasisi
ya Hassan Maajar Trust Yatoa Msaada Wa
Madawati Mkoa wa Mwanza
Tarehe 7
Mei 2013 - Mwanza.
Taasisi ya Hassan Maajar imetoa masaada
wa madawati 250 katika shule za msingi mkoa wa Mwanza.
Zaidi ya wanafunzi 700 katika
shule tano za wilaya tano ya mkoa wa Mwanza zimepokea msaada wa madawati
yaliyotolewa na Taasisi ya Hassan Maajar Trust.
Jumla ya madawati 250 yalitolea na taasisi hiyo ikiwa ni kampeni yako ya kupunguza tatizo sugu la upungufu wa madawati katika shule hizo. Hafla ya kukakabidhi madawati hao, ilifanyika katika Shule ya Msingi ya Nyaminjundu, iliyoko Wilaya ya Misungwi. Bwana Shariff Maajar, pamoja na Bi Zena M Tenga kwa niaba ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust walikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Engineer Evaristi Ndikilo.
Jumla ya madawati 250 yalitolea na taasisi hiyo ikiwa ni kampeni yako ya kupunguza tatizo sugu la upungufu wa madawati katika shule hizo. Hafla ya kukakabidhi madawati hao, ilifanyika katika Shule ya Msingi ya Nyaminjundu, iliyoko Wilaya ya Misungwi. Bwana Shariff Maajar, pamoja na Bi Zena M Tenga kwa niaba ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust walikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Engineer Evaristi Ndikilo.
“Ni adimu na mara chache kuona
Taasisi za kinyumbani za kiTanzania, kufika hapa mkoani kwetu. Kwa hiyo napenda
kutoa shukurani za dhati kwa Taasisi ya Hassan Maajar kwa msaada huu mkubwa na
wenye thamani utakaochangia kuboresha elimu katika Mkoa wetu wa Mwanza”,
alisema Engineer Ndikilo. “Kama mikoa
mengine ya nji yetu, ni wilaya na halmashauri za vijiji ambako msiaada kama hii
inaitajika kwa wingi na ni kweli kati ya changamoto nyingi zinazowakabili
watoto wetu, moja wapo ni hili la upungu wa mazingira bora ya Elimu, kwa hiyo
tunawashukuru Hassan Maajar Trust kwa kuzingatia hizi changamoto na kwa
kuufikiria mkoa wetu wa Mwanza”, aliongeza.
Huu ni msaada wa tatu chini wa
mradi wa Hassan Maajar Trust wa “Dawati Kwa Kila Mtoto”, (A Desk For Every
Child) mkoa wa Mwanza ni mko watatu kati ya mitano itakayonufaika kwa msaada
inyaotelewa na Hassan Maajar Trust kwa kutumia fedha zilizopatikana na michango
iliyotolewa kufwatia kampeni iliyoanzishwa Desemba 2011. Hadi sasa Hassan
Maajar Trust imekabidhi jumla ya madawati 1,194 kati ya madawati 1,764; Njombe
(680), Singida (264), Mwanza (250). Mikoa itayofawatia ni Lindi na Rukwa.
Garama za madawati haya ya mkoa wa Mwanza ni jumla ya Tsh 22,500,000.
“Lengo letu hususan ni kujitahidi
kuhakikisha Taasisi yetu inaboresha mazingira ya kusomea watoto katika shule
zetu Tanzania”, alisema Zena M Tenga Mkurugenzi Mtendaji. “Tunatarajia na
tunalenga kuhakikisha kuwa kampeni yetu ya Dawati Kwa Kila Mtoto inawafikia
watoto wengi iwezekenavyo na pia tutaendelea kuhamasisha jamii, taasisi tofauti
na mashirika tofauti kuendelea kutuunga mkono ilituweze kufanikisha malengo
yetu”, aliongeza.
MWISHO





.jpg)
0 comments:
Chapisha Maoni