TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 8, 2013
MIKOA YATAKIWA KUCHEZESHA COPA COCA-COLA WILAYANI
Vyama
vya Mpira wa Miguu vya mikoa vinatakiwa kuendelea na mashindano ya Copa
Coca-Cola yanayoshirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15 katika
ngazi ya wilaya wakati vikisubiriwa vifaa na fedha za uendeshaji kutoka
kwa mdhamini.
Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano (roadmap), mashindano ya Copa Coca-Cola ngazi ya wilaya yanatakiwa kufanyika na kukamilika ndani ya mwezi Mei mwaka huu ili baadaye kuendelea na hatua inayofuata.
Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano (roadmap), mashindano ya Copa Coca-Cola ngazi ya wilaya yanatakiwa kufanyika na kukamilika ndani ya mwezi Mei mwaka huu ili baadaye kuendelea na hatua inayofuata.
Hivyo,
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawataka wanachama wake
(vyama vya mpira wa miguu vya mikoa) ambao wamejipanga kuendelea na
mashindano wakati suala la vifaa na fedha likiendelea kufuatiliwa kwa
mdhamini wa mashindano.
Vifaa
na fedha zitapatikana wakati wowote baada ya taratibu husika
kukamilika. Vifaa kwa ajili ya mashindano hayo vimeagizwa kutoka nje ya
Tanzania.
Ni
matumaini yetu kuwa tutakuwa na mashindano mazuri mwaka huu
kulinganisha na msimu uliopita. Kampuni ya Coca Cola ilianza kudhamini
mashindano hayo mwaka 2007, na tangu mwaka huo yamekuwa yakifanyika kila
mwaka.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Chapisha Maoni