Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua shamba la
Minazi la Serikali la ekari 45 lililo chini ya usimamizi wa Wizara ya
Ardhi likikabidhiwa kwa Wizara ya Kilimo kwa vile lipo katika Ukanda wa
Utafiti wa Kilimo katika Kijiji cha Tumbe Mkoa Kaskazini Pemba.
Afisa
Mkuu wa Idara ya Misitu na Mali asil zisizorejesheka Pemba Nd. Said
Juma Ali akielezea hatua zilizochukuliwa na Wizara ya kilimo katika
kuotesha minazi kwenye eka 10 zilizomo ndani ya shamba la Serikali la
ekari 45 liliopo katika Kijiji cha Tumbe Kaskazini Pemba.
Sheha
wa Shehia ya Micheweni Mjini Bw. Dawa Juma Mshindo akielezea changamoto
wanazopambana nazo Masheha Kisiwani Pemba mbele ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliokutana nao katika Ukumbi wa
Chuo cha Amali Kilichopo Vitongoji vya Chake Chake Pemba.
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa uamuzi kwamba Mashamba yote ya
Mikarafuu na Minazi ya Serikali yaliyokuwa chini ya Usimamizi wa Wizara
ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati kuanzia sasa yatakuwa yakishughulikiwa
na Wziara ya Kilimo na Mali Asili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa uamuzi huo wa Serikali wakati akizungumza na Masheha wote wa Mikoa Miwili ya Pemba katika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji vya Chake Chake Pemba.
Balozi
Seif amesema wakati suala la Ardhi litaendelea kubakia Wizara ya Ardhi,
amewaomba Masheha ambao maeneo yao yamo Mashamba ya Serikali ya
Mikarafuu na Minazi na hadi sasa hayajahakikiwa watoe Taarifa kwa Afisa
Mdhamini wa Wizara ya Kilimo Pemba au Kiongozi yeyote atakayewekwa
kwenye zoni.
Ameema
udhibiti wa mapato yanayotokana na mazao yaliyomo kwenye baadhi ya
mashamba ya Serikali yalikuwa yakileta mgongano kutokana na Mashamba
hayo kushughulikiwa na Wizara mbili tofauti.
Wakielezea
changamoto zinazowakabili baadhi ya Masheha hao wamesema mazingira duni
wakati wanapostaafu utumishi wao pamoja na mfumko wa hujuma
wanazofanyiwa masheha limekuwa tatizo kubwa linalopunguza ari ya
utekelezaji wa majukumu yao.
Masheha
hao wameiomba Serikali Kuu kujenga mazingira yatakayowawezesha kupatiwa
mikopo ya vyombo vya usafiri ili kurahisisha kazi zao, masuala ambayo
Balozi Seif ameahidi kwamba Serikali itayazingatia na kuyapatia ufumbuzi
unaofaa.
Afisa
Mkuu wa Idara ya Misitu na Mali asili zisizorejesheka Pemba Nd. Said
Juma Ali alimueleza Balozi Seif kwamba Ekari kumi tayari zimeshaoteshwa
minazi mipya ya asili (East Africa).
Nd.
Ali amesema kituo cha Utafiti wa Kilimo Pemba kinaendelea na harakati
za kurejesha minazi ya asili kwa kuotesha mbegu zitakazouzwa kwa
wakulima katika maeneo mbali mbali ili kuziba pengo la minazi mipya
ambayo uzalishaji wake huchukuwa kipindi kifupi.
(Picha na habari na
Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ).
0 comments:
Chapisha Maoni