
Afisa
Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul
Mbijima akitoa somo kwa wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha
ualimu Rukwa (Rukwa Teacher's College) juu shughuli mbalimbali
zinazofanywa na mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa na mfuko huo kwa
watumishi wa Umma. Semina hiyo imeenda sambamba na maadhimisho ya wiki
ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini iliyofanyika kitaifa Mkoani Dodoma
ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete ameongoza kilele cha maadhimisho hayo jana tarehe 17.05.213.

Baadhi ya
wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa wakimsikiliza
mtoa mada kwa umakini mkubwa. Wahitimu hao ni sehemu ya wadau wakubwa
wa baadae wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

Afisa
Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul
Mbijima akiendelea na kutoa mada alizoandaa kwa wahitimu hao juu ya
umuhimu wa kujiunga na mfuko huo wenye mafao mbalimbali.

Malipo ya
uzeeni, Malipo ya ulemavu, Malipo ya mirathi, Malipo ya wategemezi, na
Malipo ya mazishi ni sehemu ya mafao muhimu yanayotolewa na mfuko huo
kwa watumishi wa umma.

Wahitimu wa
mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa wakionekana kukolea na
mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.

Afisa
Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul
Mbijima akiagana na baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu chuoni hapo
baada semina ya shughuli na mafao muhimu yanayotolewa na mfuko wa PSPF
nchini.Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
0 comments:
Chapisha Maoni