Mkuu
wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja akikagua Guard ya
Heshima iliyoandaliwa kwa ajili yake kabla ya kuanza zoezi la Uvalisha
Nishani kwa Maafisa na Askari wa Magereza toka Mikoa ya Kanda ya
Kaskazini leo Mei 28, 2013 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi,
Kilimanjaro.
Mkuu
wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (kulia) akimvalisha
Nishani ya Utumishi Uliotukuka Kazini, Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Kilimanjaro, ACP Hamis Nkubasi. Jumla ya Maafisa na Askari 30 kutoka
Mikoa ya Kanda ya Kaskazini wamevalishwa Nishani mbalimbali leo, Mei 28,
2013 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro.
Guard
Maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima kwa Mkuu wa Jeshi la
Magereza, Kamishna Jenerali John Minja (hayupo pichani) ikitoa heshima
kabla ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la
Magereza wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini lililofanyika leo Mei 28, 2013
katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro.
Mkuu
wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (katikati waliokaa)
akiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa Nishani mara baada ya zoezi
la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka
Mikoa ya Kanda ya Kaskazini leo Mei 28, 2013 katika viwanja vya Gereza
Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro.
Picha na Felix Mwagara.
Picha na Felix Mwagara.
0 comments:
Chapisha Maoni