Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi
akizungumza na mmojawapo wa Wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya waliofanya
kikao naye jijini Dar es Salaam Katikati ni Mkuu wa Jeshi la Polisi IJP Said Mwema.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi
katika Kikao na Wawakilishi wa Nchi za Umoja wa Ulaya waliomtembelea
Wizarani.. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mbarak Abdulwakil.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IJP Said Mwema pia alihudhuria
Kikao hicho akiwa na Wakuu wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam
(Kushoto).Picha zote na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi
---
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel nchimbi
amesema Serikali imeimarisha shughuli za ulinzi hapa nchini ili kuhakikisha
kuwa wananchi na wageni wanaishi na kufanya shughuli zao kwa amani.
Dk. Nchimbi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam
alipokutana na Ujumbe wa wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU)
na baadhi ya mabalozi wa Nchi hizo waliopo hapa nchini.
Aliuambia ujumbe huo ulioongozwa na Balozi Filberto
Cerani Sebregondi kuwa Jeshi la Polisi limeweka mikakati mbalimbali
ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika jiji la Dar es Salaam na
maeneo mengine ya nchi.
Amesema kwa upande wa raia wa kigeni, Jeshi hilo
limeanzisha Dawati Maalumu litakalohudumia raia hao pale wanapopata
matatizo ili waweze kupata huduma za haraka.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Ujumbe huo amesema
Umoja huo utaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
na ameishukuru Wizara hiyo kwa jitihada inazoendelea kuchukua kuhakikisha
ulinzi na usalama unaimarishwa kwa wageni na raia.
0 comments:
Chapisha Maoni