WAZIRI WILLIAM LUKUVI.
Akisoma ripoti hiyo kwa niaba ya waziri mkuu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu mheshimiwa WILLIAM LUKUVI amesema kamati ya bunge iliyoundwa kuchunguza chanzo cha matatizo ya kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka 2012 tayari imewasilisha ripoti kwa baraza la mawaziri na mapendekezo ya nini kifanyike ambapo baraza la mawaziri limeridhia mambo yafuatayo kufanywa kwa haraka kama ifuatavyo:-
1.MATOKEO YOTE YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 YAFUTWE NA YAANDALIWE UPYA KWA KUTUMIA UTARATIBU ULIOTUMIKA MWAKA 2011.
2.STANDARDIZATION IFANYIKE ILI MATOKEO YA WANAFUNZI YALINGANE NA JUHUDI WALIZOZIWEKA KATIKA KUSOMA KULINGANA NA MAZINGIRA YA TANZANIA.
3.BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA LIMEELEKEZWA KUWASHIRIKISHA WADAU WOTE WA ELIMU WAKATI WAKIPANGA MAREKEBISHO YOYOTE YA KUPANGA VIWANGO VYA UFAULU WA MADARAJA YA UFAULU NA KUFUTWA MARA MOJA UTARATIBU ULIOTUMIKA 2012 KUPANGA VIWANGO HIVYO NA MCHAKATO WA KUTOA MATOKEO MAPYA UANZE MARA MOJA.
NB.KUTOKANA NA UMUHIMU WA MAPENDEKEZO HAYA YA TUME BARAZA LA MAWAZIRI LIMEAMUA UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO HAYA UFANYIKE MARA MOJA.
0 comments:
Chapisha Maoni