KAMANDA MWAKALINGA AKIONYESHA RISASI WALIZOKAMATWA NAZO MAJAMBAZI HAO.
MMOJA WA WATUHUMIWA HAO WA UJAMBAZI AKIWA HOSIPTALINI BAADA YA KUNUSURIKA KIFO BAADA YA KIPIGO KUTOKA KWA WANANCHI
WANANCHI WAKIWA HOSIPTALINI KUSHUHUDIA MAJAMBAZI HAO NA KUWATAMBUA.
JAMBAZI JINGINE HILO LIKIWA HOI BAADA YA KIPIGO KIKALI KUTOKA KWA WANANCHI AKIWA HOSIPTALINI
Jeshi la Polisi Mkoani Lindi linawashikilia watu wawili kwa Tuhuma za Unyanganyi kwa kutumia silaha na kujeruhi Mfanyabiasha wa Duka katika kijiji Cha Kitomanga Wilayani Lindi huku wakiwa katika hospital ya Mkoa baada ya kunusurika kufa kufuatia Wananchi wenye hasira kutaka kuwaua kwa kuwachoma Moto
Akiongea na waandishi wa habari Ofisi kwake hii leo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,George Mwakajinga alieleza kuwa Watuhumiwa hao waliojitambulisha kwa Rajabu Juma Mbete(26) mkazi wa manispaa ya Lindi na Hamis Athuman(32) mkazi wa Mbembetini Kibiti Mkoani Pwani licha ya kupora simu 6 na fedha taslim laki 6 pia walimjeruhi kwa Mapanga Bw Hamis Hassan Muuza duka hilo Mwakajinga alibainisha kuwa Majambazi hayo yanayosadikiwa kuwa 4 walifanikiwa kukimbia baada ya Bunduki waliyokuwa nayo kugoma kufyetua risasi hali iliyofanya wanavijiji vya Kitomanga,Mkwajuni na Mbwemkuru
kuanza msako na kufanikiwa kuwakamata na kuwajeruhi kwa kuwapiga na kuwachoma moto kabla hawajapata msaada wa Jeshi la Polisi
Akielezea kuhusu kukutwa na risasi tatu za Shortgun,Bangi pamoja na Bunduki aina ya Shortgun ya kienyeji, Kamanda mwakajinga alifafanua kuwa Bunduki hiyo pia hutumia risasi za Short gun
ambapo pia walikutwa na risasi 3
Kufuatia kukamatwa kwa majambazi hao baadhi ya Wafanyabiashara wa Manispaa ya Lindi akiwemo Seif Nasor na Ahmaid Nachuli wameeleza kuwa tatizo la kuongezeka kwa majambazi kunachangiwa na Uozo wa sheria hali inayosababisha jamii kujichulia sheria mkononi
Watuhumiwa hao ambao wamelazwa huku wakiwa chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi watafikishwa mhakamani mara baada ya Afya yao Kuimarika kutokana na kunusurika kuchomwa Moto na Wananchi ambapo tayari wameweza kutambuliwa na baadhi ya wanakijiji

0 comments:
Chapisha Maoni