Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (mbele) akiwa na Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Njombe, Deo Sanga, wakikagua hali ya usalama na amani katika
mwambao wa Ziwa Nyasa eneo la Lupingu wakati wa ziara ya kikazi ya
siku saba ya kuimarisha uhai wa chama hicho mkoani Njombe leo.
PICHA
ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wa pili kulia) akiwa na Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (mbele) wakikagua hali ya
usalama na amani katika
mwambao wa Ziwa Nyasa eneo la Lupingu wakati wa ziara ya kikazi ya
siku saba ya kuimarisha uhai wa chama hicho mkoani Njombe. Kushoto
ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe na Mbunge wa Mwibara,
Kange Lugora.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akimsadia Agnes Haule
kutwanga mhogo alipomkuta akitwanga katika Kijiji cha Lupingu, Ludewa
leo.
Kikundi la ngoma ya mganda kikitumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara
uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Kijiji cha
Lupingu, mwambao wa Ziwa Nyasa, Ludewa.
Mbunge wa Mwibara, mkoani Mara, Kange Lugora akiungana na Consolata Kayombo kucheza noma ya Chioda wakati wa mkutano huo.
Wananchi wa Lupingu, mwambao wa Ziwa Nyasa wakimbeba Mbunge wa Jimbo hilo, Deo Filikunjmbe wakati wa mkutano huo.
Wananchi wakila kiapo cha utii cha CCM wakati wa mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM, AKinana akijadiliana jambo na Mbunge wa Lu, Deo Filikunjombe baada ya kumaiziza kuhutubia mkutano wa hadhara
0 comments:
Chapisha Maoni