Searching...
Jumatatu, 6 Mei 2013

KENYA YAWAHUKUMU WAIRANI WAWILI KIFUNGO CHA MAISHA JELA.

 
Bwana Ahmad Mohammed na Sayed Mousaviwakiwa mahakamani kenya kabla ya kuhukumiwa kifungo cha maisha jela
 Raia wawili wa Iran wamehukumiwa kifungo cha maisha katika mahakama moja ya Kenya kuhusiana na mashtaka ya ugaidi.
Raia hao ni Ahmad Mohammed na Sayed Mousavi ambao walishtakiwa wiki iliyopita kwa kumiliki vilipuzi, ambavyo inaaminika vilikuwa vitumiwe kwa kufanya mashambulizi.
"mwili unanisisimka nikifikiria hasara ambayo ingesababishwa na shambulizi hilo la kigaidi," amesema jaji Kiarie Waweru Kiarie wakati akitoa hukumu hiyo.
Hata hivyo, serikali ya Iran imekana kuhusika na mpango huo wa kuishambulia nchi ya Kenya.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!