Searching...
Ijumaa, 17 Mei 2013

JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA LIMETOA TAARIFA YA DAWATI LA JINSIA

Dawati la jinsia la jeshi la polisi mkoani Iringa limepokea kesi 592 kwa mienzi mitatu ndani ya mwaka huu zikiwemo kesi za watoto,wanawake na wanaume.

Akizungumza kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amezitaja kesi hizo kwa upande wa watoto ni kesi za kubaka ni 24,kesi za kufanya mapenzi na wanafunzi 3,kumpa mimba mwanafunzi 5,kutorosha wanafunzi 5,kutupa watoto 4,kulawiti 1,shambulio la kudhuru mwili 13,kujeruhi 1 na shambulio la aibu kesi 1.


Kwa upande wa kesi za wanawake katika dawati hilo ni kubaka 4,kujeruhi 46,kutumia ruga ya matusi 26,kutishia kuua kwa maneno na sms kesi 46,kutishia kuua kwa vitu nyenye ncha kali kesi 22,kutelekeza familia kesi 14 na shambulio la kudhulu mwili kesi 162.

Hata hivyo katika upande wa wanaume kesi walizopokea ni kesi ya kujeruhi 57,kutumia lugha za matusi kesi 20,kutishia kuua kwa maneno na sms kesi 30,kutishia kuua kwa vitu vyenye ncha kali kesi 11 na shambulio la kudhulu mwili kesi 97.

Aidha kamanda ameongeza kwa kusema kuwa mbali na elimu kuendelea kutolewa bado dawati hilo linachangamoto ya mwitikio kwa upande wa wanaume katika kwenda kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa vitendo vya kinyama na wake zao.

0 comments:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Back to top!