Mlinzi
wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya
Morogoro Dar es salaam jirani na daraja la Mzambarauni Bw
Mika Athumani amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.Habari
zilizoptaikana eneo la tukio zilidai kwamba majambazi hao baada ya
kuvamia baa hiyo iliyojitenga usiku wa manane na kumvamia mlinzi huyo
na kumchinja kama kuku na baadae kuvunja baa hiyo na kuimba vitu mbali
mbali.
Akihojiwa
na blog hii mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi alidai
kwamba majambazi hao walimvamia mlinzi wake na kumchinja na baadae
walivunja Counter ya baa hiyo pamoja na duka lililopo jirani na baa hiyo
na kuiba vitu mbali mbali.Alipoulizwa
kwamba kuna taarifa zinadai kwamba mlinzi huyo alikutwa akiwa amelala
Bw Mushi alisema inawezekana lakini
hakuna mtu mwenye uhakika na jambo hilo kwani sote hatukuwepo,wakati
tukio hilo linatokea"alisema Bw Mushi ambaye anadai bado hajafahami
dhamani ya vitu vilivyoibikiwa na majambazi hayo.
Mwananachi akishuhudia damu ya mlinzi huyo kwa hudhuni
Baskeli ya Mlinzi huyo ikiwa imetapakaa damu ambapo inadaiwa mlinzi huyo alikuwa amelala kwenye eneo hilo
Redio ambayo majambazi hayo waliiangusha nje ya baa hiyo
Majira
ya saa 12 asubuhi ya leo wananchi walishuhudia maduka mawili ya baa
hiyo yakiwa wazi huku mwili wa mlinzi huyo umekutwa upande wa baa ukiwa
umechinjwa na kutenganishwa kichwa na mwili
Umati wa watu ukishuhudia tukio hilo muda mfupi uliopita.
Gari la polisi likiondoka eneo la tukio na mwili wa marehemu
Wananchi nao waliondoka eneo hilo la tukio.
Mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi akihojiwa na waandishi wa habari eneo la tukio.
Majirani wa eneo hilo wakihojiwa na waandishi wa habari
Baadhi
ya watu waliokuwepo eneo hilo la tukio walidai kwamba mlinzi huyo
alikuwa amelala hivyo majambazi hayo yalimvamia na kumpora silaha zake
na kisha kumchinja shingoni," siumeona alikuwa amelala jirani na
baiskeli yake ndio maana ameshindwa kupambana nao hasa ukizingatia baa
hii imejitenga iko peke yake hapa jirani na mto wa Morogoro"alisema Bw
Maneo Mashani.
Mtandao
huu ulishuhudia mtoto wa marehemu pamoja na mjukuu wa marehemu
wakiangua vilio eneo la tuko baada ya kuuona mwili wa marehemu
aliyeuwawa kikatili baadae wote wawili walipanda gari la polisi na
kuondoka nao.
0 comments:
Chapisha Maoni