Picha
juu na chini ni Foleni ya magari ya takataka zaidi ya 30 yaliyokwama
katika dampo la Pugu Kinyamwezi kwa takribani siku tatu kutokana na
ubovu wa miundo mbinu huku taka zikiendelea kuoza ndani ya magari hayo
na kusababisha harufu mbaya kwa wakazi wa maeneo hayo.
Katapila likiwa katika jitihada za kuchonga barabara ili angalau magari ya taka yaweze kufika eneo la dampo kuwamga taka.
Masela wakifurahia baada ya gari la
taka lililokuwa limekwama kufanikiwa kupandisha kilima katika dampo hilo
kuelekea kumwaga taka.
Wanafunzi wa shule ya msingi
walipokutwa na camera yetu katika dampo hilo wakikatiza na kuzubaa zubaa
eneo hilo wakati wa saa za shule.
Wakazi wa maeneo hayo wakichambua
takataka hizo kujiokotea chupa tupu za maji na mifuko ya plastiki ikiwa
ni ajira waliyojitengenezea katika kuendesha maisha yao ya kila siku,
shuhuda wa Mo Blog Zainul Mzige anatanabaisha kwamba chupa wanazookota
huuzwa kilo moja kwa shilingi 100 kitu kinachowapelekea wafanyaji wa
biashara hii kuwa watumwa wa pombe za kienyeji haswa almaarufu kama
Gongo au Chang'aa.
Mitaro ya maji machafu ikiwemo mikojo na vinyesi katika dampo hilo...Je kuna kupona kweli hapa????
Magari ya Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni nayo yalikwama kwenye dampo hilo, pichani yakielekea kuwamga
taka hizo baada ya barabara kutengemaa kwa kiasi.
Pichani ni juu na chini Mama lishe
wakitoa huduma ya chakula chini ya mti katika eneo lilizongukwa na taka
ikiwemo harufu kali na Nzi wanaozunguka hapa na pale lakini vibarua wa
dampo hilo hawana la kufanya.
Moja
ya Katapila lililokodiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam
likiwa limekufa na kushindwa kufanya kazi kutokana na kukwamisha na
miundo mbinu ya eneo hilo la dampo huku mafundi wakihangaika kulifufua.
Meneja
wa Dampo la Pugu Kinyamwezi Bw. Richard Katiti akizungumzia changamoto
kubwa wanayokabiliana nayo katika kipindi hiki cha mvua kitu ambacho
kinawapelekea kutumia jitihada za ziada ikiwemo kukodisha magari
(Vijiko) ili kujitahidi kuhakikisha miundo mbinu ya kufika katika dampo
hili inapitika kwa urahisi ili kuondoa vikwazo kwa magari yanayotoa
huduma ya kuzoa taka mjini.
Devera
wa gari la Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Ramadhani Sufi
akielezea adha wanayoipata ambapo amefafanua kuwa inafika mahali
inawabidi kulala siku mbili na gari zenye mzigo wa taka katika mazingira
ambayo ndio wanayoshinda na kula kitu ambacho kinaweza kuwasabishia
maradhi hivyo ameliomba jiji kurekebisha hali hiyo ili kuwaepusha na
mazingira hatarishi kiafya kutokana na uchafu unaolundikana mahali
pamoja kuanzia dampo hadi kwenye magari.
Aidha amefafanua kuwa hali hiyo
inasababisha kutuchafulia jina la kampuni yetu na kuonekana kama
hatufanyi kazi kumbe tatizo lipo kwenye utaratibu mzima wa Manispaa na
suala la miundo mbinu.
Pia ameshauri jiji liongezewe uwezo
kutokana na kuwa na vyombo vichache na chakavu kitu kinachopelekea
kuzidiwa katika kutoa huduma katika dampo hilo.
Mmoja wa madereva wa magari ya taka
yaliyokwama kutokana na miundo mbinu mibovu Bw. Frank John akielezea
kero ya kwenye dampo la taka lililopo maeneo ya Pugu Kinyamwezi ambapo
amesema taka zimelundikana barabara hazipitiki hata magreda ya kuzoa
hayana pakupita na kuwaomba watu wanaohusika na dampo kujaribu
kutengeneza njia mbadala na kushauri itafutwe njia kipindi cha Masika
taka ziwe zinamwaga sehemu nyingine na kipindi cha Kiangazi kiwe na
sehemu yake na kushauri mamlaka zinazohusika na usafi zijifunze kutoka
kwa wananchi na sisi tujifunze kutoka kwao.
Aidha Bw. John amewataka viongozi
wahusika kutokaa maofisini na kutembelea maeneo husika na kujiuliza
kwanini gari zinakwama na kuongeza kuwa tatizo hilo limepelekea lawama
kwa baadhi kampuni za usafi kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kila
siku kwa wakati.
Hii ndio hali halisi ya viroba vya
uchafu vilivyolundikwa katika eneo la Pugu Kwalala pembezoni mwa
barabara na makazi ya watu ambapo wananchi wamekuwa wakizilalamikia kwa
sababu kipindi cha mvua vinaweza kuwasababishia magonjwa ya milipuko
ikiwemo Kipindupindu.
Mkazi wa eneo la Gongo Mwisho wa
lami - Pugu Kwalala Bw.Erasto Njau akilalamikia ubovu wa magari ya taka
ya Halmashauri ya Manispaa ya jiji la Dar es Salaam na vile vile
utaratibu mbovu wa ukusanyaji wa taka ambapo hata kama gari imeharibika
yangetumika magari mengine kuja kubeba taka suala ambalo linalohusu
uongozi wa Manispaa ambao ndio unaogharamia magari yanayobeba taka kitu
ambacho kinaonyesha utaratibu wa ubebaji taka bado haujakaa sawa.
Mama Lishe Asha Omari Dundo akizungumzia
kero ya Mlundikano wa taka katika eneo lake la biashara ambalo sio
dampo rasmi la kutupia takataka na anapouliza anaambiwa magari yamekwama
dampo kutokana na ubovu wa miundo mbinu kitu ambacho ni hatari kiafya
kwa wateja wake wa chakula ambacho ndio biashara anayoifanya kwa ajili
ya kusomesha watoto na kila anapouliza hapewi jibu linaloeleweka na
ameiomba serikali kutupia macho swala hilo kwa sababu kumekuwa na kauli
tofauti malori yamekwama na malori mabovu.
Mama Lishe Asha Omari Dundo akiwaandalia wateja wake chakula cha mchana katika eneo ambalo ni hatarishi kwa walaji.
Mkuu wa Afya Mazingira wa
Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam Bw. Membe Protus Membe
akizungumzia jitihada za Manispaa katika kupambana na tatizo la
mlundikano wa magari ya taka yaliyokwama katika eneo la Dampo la Pugu
Kinyamwezi kutokana na ubovu miundo mbinu ya barabara unaopelekea
kukwamisha zoezi la ukusanyaji taka katika maeneo mbalimbali ya jiji la
Dar na kusababisha mlundikano wa taka nyingi kwa muda wa kipindi cha
siku hizi tatu.
Hata hiyvo amesema katika muda wa
siku tatu kuanzia leo Manispaa itahakikisha inarekebisha miundo mbinu ya
kuelekea dampo ili kuweza kupunguza msongamano uliopo wa magari ya taka
yaliyokwama yaweze kurudi mjini kuendelea na ubebaji wa taka.
Aidha Bw. Membe ameahidi kuwa
shughuli za umwagaji taka katika dampo hilo zitakuwa zikifanyika mchana
na usiku ili kuondoa mlundikano wa taka mitaani ambao umejitokeza katika
muda wa siku tatu
0 comments:
Chapisha Maoni